

[KANUNI ZA KUTEKA MIJI KWA
AJILI YA BWANA, KWA NJIA YA
MAOMBI.TOLEO LA PILI 2012
]
UTANGULIZI
Ndugu mpendwa
napenda kukusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Pia ninapenda
kukukaribisha katika kujifunza somo hili.Somo hili lina umuhimu mkubwa sana
katika nyakati/majira tuliyopo
sasa.Kama kichwa cha somo kinavyoonyesha,somo hili ni somo ambalo naamini
litakwenda kuleta mapinduzi ya kiroho katika jamii,familia na kanisa kwa
ujumla.Nakushauri ulisome somo hili kwa mtiririko ili uweze kupata maarifa
mapya na vitu vipya kutoka kwa Roho Mtakatifu.Lengo la kwanza la somo hili ni
kukuandaa kama mwanajeshi wa Bwana,kwa ajili ya kuteka miji iliyo chini ya
shetani na kuirejeza kwenye ufalme wa Mungu Baba.Sasa unaweza ukawa
unajiuliza,swali hili;kwamba kwa nini mimi ndio niteke miji hiyo?kwanini Mungu
mwenyewe asifanye kazi hiyo?Jibu ni kwamba Mungu huwa anafanya kazi pamoja nasi
kwa ajili ya kutupatia mema[Rumi.8:28],Na
mema hayawezi kuja kama miji tunayoishi itaendelea kuwa chini ya ufalme wa
giza.Kwa nini tuteke miji wakati,aliyeumba miji yote ni Mungu na wala sio shetani?
Dhambi ya Adamu
na Eva pale eden ilipelekea dunia yote kuwa chini ya shetani(yaani shetani
akawa ndio mungu wa dunia hii)[2kor.4:4]
badala ya mwanadamu. Kwa hiyo asilimia kubwa ya miji tunayoishi inamilikiwa na
adui(shetani).Na ndio maana kazi ya Mungu inapigwa vita kwa kiasi kikubwa.Sasa
lengo la pili la somo hili ni kukuwekea(impart knowledge) ufahamu
utakaokusaidia kuirejeza miji hiyo mikononi mwako,kama mwakilishi wa ufalme wa
Mungu.Kutokana na miji mingi kuwa chini ya shetani,matukio mengi ya kutisha
yamekuwa yakitokea kila siku,mfano vifo vya ajabu,ajali za barabarani,mauaji ya
albino nk.
Sasa shetani amekuwa akipofusha watu ili watu wasijue kuwa yeye(shetani)
ndiye anayehusika katika matukio hayo yasiyo na hata chembe ya huruma[Mungu ni
mwenye huruma] hawezi amuru maalbino wauae,ajali za watu kufa kama vile kuku
kwa mkupuo.Ndugu mpendwa shetani ni mjanja na biblia inasema kwenye kitabu cha
ufunuo kuwa anajua wakati uliobaki ni mchache..kwa hiyo anachofanya ni
kuhakikisha anav
Ni
muda mrefu sana nimekuwa nikisikia matukio mengi ya kutisha na ya ajabu yakitokea katika jamii tunazoishi;
hasahasa matukio ya ajali za barabarani, ukatili , watu kujinyonga na kunywa
sumu nk.Na mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wengi wakisema yote hayo ni
mapenzi ya Mungu(yaani Mungu ndio amesababisha) na muda mwingine hata watumishi
wa Mungu wengi wakati wa mazishi nimewasikia na wewe umewasikia wakisema “Bwana
ametoa na Bwana ametwaa;jina la Bwana libarikiwe”
Kwa upande wangu nimekuwa nikipata shida kidogo juu ya misemo hii ya mazishi, na Je ni kweli Bwana ndiye
anayetwaa hao watu wote? mfano mlevi,ajali nk.Maana muda mwingine unakuta wala
Mungu hahusiki hata kidogo katika matukio hayo, bali aiza mtu amejisababishia
mwenyewe au kuna mkono wa shetani umehusika!.Si kwamba nasema Mungu hahusiki
kwa asilimia zote,hapana!.Bali ukikuta Mungu amehusika basi mtu huyo amekuwa
mgumu sana na amekuwa akiharibu kazi ya Mungu mfano,Herode[Matendo.12:22-23] au Mungu amependa kumpumzisha mtu huyo kwasababu
ya umri[1Fal.1:1,1nyak.29:28 .
Kumbuka kuwa si mapenzi ya Mungu mtu afe katika dhambi[Eze.18:23; 33:11], pia si mapenzi ya Mungu ufe kabla ya wakati
ambao yeye amekusudia uishi hapa duniani ambao ni miaka 120[Mwanzo.6:3] kama ukiishi vizuri na
Bwana hiki ni kiwango cha chini tu unaweza ukaishi zaidi ya hapo mfano ibrahimu
aliishi miaka 140,Ayubu 140.Sasa kama ndio hivyo kwa nini uondoke kabla ya
hapo.
Sio hivyo tu bali kwa wewe mtumishi wa Mungu uwepo wako hapa duniani ni
wa muhimu sana,Yesu alimwomba Baba wa mbinguni ili asitutoe ulimwenguni [Yoh.17:15] , maana yake kuna kazi
unatakiwa ufanye,na endapo utaonekana huifanyi na wala humzalii Mungu matunda
basi ndio unakatwa[Math.3:11,7:19;
Luka.13:6-9](sasa hii ni kwa ajili ya wale tu ya waliokoka).ni kweli kufa
ni faida kwa mtu aliyeokoka,hilo nakubaliana nalo asilimia zote,lakini pia
kuishi ni kristo na kwafaa sana kubaki kwa ajili ya kristo na ili kuendelea
kuziremba taji zetu za kule mbinguni(kumbuka kuwa utalipwa kwa ajili ya kazi
unayofanya hapa Duniani,utavalishwa taji,kama ukienda huko na hakuna matunda
yoyote uliyomzalia Mungu basi usitarajie kitu.
Unajua
utakuwaje?Embu fikiria unahitimu kidato cha 4/6 au chuo alafu siku hiyo wenzako
wote wanapewa zawadi na kuvalishwa taji, alafu wewe peke yako tu ,ndio huna mtu
wa kukuvalisha taji wala kukupa zawadi,unafikiri utajisikiaje?lazima ujisikie
vibaya.Ndivyo itakavyokuwa unavyong’ang’ania kufa ukisema ni faida wakati hamna
chochote ulichokifanya hapa duniani kwa ajili ya Mungu[Luka.12:47-48].
Ujue hii
inakuhusu wewe ndugu uliyeokoka na lengo langu hapa ni kuona unabadilisha
mawazo uliyonayo na maombi ambayo umekuwa ukimwomba Mungu ili akuondoe
duniani.Kumbuka kuwa Mungu anakuhitaji ili uendelee kuwepo hapa duniani kwa
aijli ya kazi yake[Yoh.17:15].Wewe
ukifa shetani anafurahia kwa sababu upinzani unapungua.Hivyo badilisha hayo
mawazo ya kutaka kuondoka(kufa) bali umwombe Mungu akuongezee siku za kuishi
angalau na wewe ujitengenezee taji yako kule mbinguni[Ufunuo.2,3].
Sasa kwa watu ambao hawajaokoka Mungu anasema anachukia kufa kwao katika
dhambi,na kwasababu hiyo basi inamanisha kuwa Mungu hahusiki katika vifo vingi
vya watu wanaokufa kabla ya wakati uliokusudiwa.Na ukijaribu kuchunguza kwa
undani zaidi utakuta asilmia kubwa ya ajali na vifo vinavyotokea nyakati za
leo, wala Mungu hahusiki na kama anahusika naweza nikasema kuwa ni kwa asilimia
chache sana( 25%) tu tena hiki ni kiwango kikubwa sana.Embu fikiria vifo vya maalibino,watoto wachanga,vijana
wadogo,Ajali za kila siku barabarani na watu kujinyonga na kunywa sumu je haya
yote utasema Mungu anahusika?
Sasa usishtuke maana lengo la somo hili sio kukuogopesha bali somo hili
lengo lake kubwa ni kufuta mawazo hasi(potofu) uliyojengewa na watu kuhusu
masuala hayo na upate ufahamu mpya(chanya) ili uweze kuchukua hatua ambazo
Mungu anataka wewe uzichukue ili angalau wewe uweze fikisha siku za Bwana.
NB:Kuna watu ambao mmekuwa na mawazo potofu,eti kwamba ukifundisha
mafundisho kama haya una mtukuza shetani sana kwasababu yeye ndiye anatajwa
mara nyingi.Nani kakudanganya kuwa unapomtaja mtu kwa ubaya,kwa lengo la
kufichua maovu yake,ni kwamba unamsifia?.Siri ya vita vyote sikuzote ni kumsoma
adui yako na kumsoma adui yako haimaanishi unamtukuza.Ndugu kama na wew ulikuwa
na mawazo kama haya uyaondoe,maana hayatoki kwa Mungu bali kwa shetani ; kwa
lengo la kukufanya usizijue hila zake na ili aendelee kukutawala na kutawala
mji unaoishi.
Kanuni ya kusoma somo hili ni kwamba kabla haujaendelea na somo hili
nakusihi ufanye maombi kwanza umuombe Roho mtakatifu akupe kiu ya kujifunza
somo hili na nguvu ya kulitendea kazi [soma Mt.7:24-27; 13:18-23] maana somo hili lina upinzani sana.mpaka
nimeweza kuliandaa somo hili ni kwa neema ya Mungu tu na kama sio neema hiyo
basi sasa hivi usingekuwa na nakala hii.Hivyo anza kwa maombi,haribu na uvunje
kila roho zilizotumwa na mwovu ili kukuzuia usipate kitu katika somo hili.Pia
uwe na biblia yako karibu.Somo hili limegawanyika katika sehemu kuu tano (5);
sehemu ya kwanza ,ya pili ,ya tatu,nne,tano na hitimisho.
SEHEMU YA KWANZA:KUJITAMBUA NA KUTAMBUA
Somo hili
limekuja wakati muafaka ambao wewe kama mtu wa Mungu unatakiwa ujitambue wewe
ni nani,unapambana nanani(adui)? ;na ni nini unatakiwa kufanya katika nyakati
hizi za mwisho.
Tunaposema kujitambua inamaanisha kuwa wewe mtu wa Mungu unatakiwa
kujitambua kuwa wewe ni nani mbele za Mungu na nini unatakiwa kufanya.Na
tunaposema kutambua maana yake unapaswa kujua adui yako ni nani?,na ni majira
gani uliyoko?
Na nianze kwa kusema kwamba shida kubwa iliyoko katikati ya wana wa
Mungu(waliookoka) ni kutokujua majira waliyoko na hata kama wanajua wanashindwa
kutambua ninini wanachotakiwa kufanya kwenye majira hayo[Efeso.5:15-21].Wapendwa wengi nyakati za leo wamejikita zaidi
kwenye kuombea masuala ya kwao na ya madhehebu ya kwao.Wamesahau kuwa nini Yesu
aliwaagiza(The great commission)
[Mathayo.24:14]..Kumbuka kuwa Yesu
alisema kwamba ; “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…na kuwafundisha
kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..”[Mathayo.28:19-20].
Lakini wapendwa wengi swala hili hawana mpango nalo ,badala yake
wamegeuka na kuwa kama wanasiasa ambao badala ya kuwatetea wananchi waliowachagua,wananza kutetea vyama
vyao;na ndivyo walivyo watumishi na wapendwa wengi wa leo.badala ya kumtetea
Yesu aliyewatuma wanaanza kutetea madhehebu ya yao.Hii yote ni kutokujitambua
na kutokutambua
mapenzi ya Bwana wao[Luka.12:47-48].
Biblia inasema
katika kitabu cha [Ufunuo.12:12b].“Ole wa nchi na bahari! kwa maana yule ibilisi ameshuka
kwenu mwenye ghadhabu nyingi ,akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”Biblia
inaweka wazi kuwa shetani yeye anajua majira aliyoko na anayatumia
vizuri…Kanisa la leo limesahau na hata kama halijasahau basi limeacha wajibu
wake na kazi ambayo Mungu alikusudia kanisa lifanye(The great commission)[Mathayo.24:14].
Kila kanisa(madhehebu) leo hii, limejiwekea vipao mbele vyake katika
mambo yao.Lakini masuala ya Mungu wameyaweka pembeni.Kanisa la leo halina muda
wa kutafuta mapenzi ya Mungu.Ukikuta mipango wanayopanga ni ya kwao binafsi na
hata ukikuta mahubiri wanayoyafundisha ni ya kusengenya kanisa
lingine,wakifikiri kuwa wanapatia kumbe wanakosea w.Kanisa la mitume halikuwa
na tabia hizi za leo.
Na kwa sababu
hiyo tunahitaji matenge wanasahau kuwa Yesu alisema; “……na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru ninyi..”[Mathayo.28:19-20]
ikiwemo upedo[Yoh.13:34-35],kupenda
jirani na Adui yako[Matthayo.5:43-48].Kanisa
la leo linahitaji matengenezo(reformation) mapya kama yale aliyoyafanya
mtumishi wa Mungu Martin Luther.Kanisa
la leo halina umoja,halina upendo, halina unyenyekevu ,wala uvumilivu na
kusamehana nk.Zaidi sana ubinafsi na kusengenyana ndio kumejaa makanisani
Kwakweli kanisa linapaswa kutubu na kurudi kwenye kusudi ambalo Mungu
alikusudia kanisa lifanye.
Sasa unaweza
ukaanza kufikiria kuwa ninalalama bure hapana! Ila nakufundisha kitu ambacho
kipo kwenye biblia.Wala sio
nimebuni.sasa tufuatane nikupitishe kwenye maandiko ili upate kujua nini ,Mungu
alikusudia kwa ajili ya kanisa;alafu linganisha na jinsi kanisa la leo
linavyoishi.Sasa tuanzie mwanzo kabisa wa nini ambacho Mungu alikuwa anakusudia
kwa ajili ya kanisa:-
Kitabu cha [mwanzo.1:26-28] kinaonyesha mwanzo wa
uumbaji wa Mungu wa kumuumba mwanadamu.Mungu anasema ″Na tufanye mtu kwa mfano wetu ;na
kwa sura yetu ;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani ;na wanyama ;na
nchi yote pia;na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi……″
Lengo kubwa la Mungu kuumba Dunia ni kwa ajili ya
mwanadamu na ndio maana aliweka kila kitu cha kumsaidia na cha kumfaa mwanadamu
katika maisha yake ;kabla hajaumbwa aliwekewa hewa
–oksjeni;maji;miti;mifugo;mimea n.k.Vyote hivi ni kwa ajili ya mwanadamu.
Na baada ya Bwana Mungu kumuumba
mwanadamu alimkabidhi utawala na umiliki wa Dunia hii.Alipewa kumiliki dunia na
vyote vilivyomo ndani yake- [Mwanzo1:
27-28].“Mungu akawabarikia……na
kuitiisha ;mkatawale……na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi ″.Neno
ninalotaka ulione hapo kwenye mistari hiyo ni “kutiisha na kutawala dunia”
Wakati huohuo ndani ya Dunia pia alikuwemo shetan, kwa sababu tayari
alishahasi kule mbinguni na akatupwa Duniani.soma-[Isaya.14:12-15,Eze.28:11-19].
[Ufunuo. 12:10.]“………kwa maana ametupwa chini
mshitaki wa ndugu zetu, yeye
awashitakiye mbele za Mungu wet,u mchana na usiku ″.
Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa nafasi moja ya heshima na kubwa sana
–na nafasi hiyo ni ya umiliki wa
Dunia hii-Na kwa ujumla hakuna malaika yeyote aliyewahi kupewa nafasi kama
aliyopewa mwanadamu,hata shetani enzi za uhai wake (kule mbinguni) hakuwahi
kupata nafasi kama hiyo, japo aliitamani sana na ndio maana alifanya uhasi
akifikiri kuwa angepata sehemu ya kumiliki, na yeye awe kama Mungu.
Katika
ranking(ngazi) ya ufalme wa Mungu hapa duniani, mwanadamu alipewa nafasi ya
pili-yaani baada ya Mungu alifuata mwanadamu;alafu malaika na mwisho ni shetani
na mapepo yake . Tazama mchoro huu
hapo chini:-
MUNGU
BABA+MWANA +ROHO MTAKATIFU
|
↓
MWANADAMU
MME + MKE
|
↓
MALAIKA
|
Shetani
|
A:
Mwanadamu.
i)Zab.8:4-6:
″…….umemfanya
mdogo punde kuliko Mungu…umevitia vitu
vyote chini ya miguu yake………Ndege wa angani………..na kila kipitacho njia za baharini. ″
ii)Ebrania
2:7
″………″umemfanya
mdogo punde kuliko malaika umemvika taji ya utukufu na heshima………″
-Maandiko yote hapo juu yanaonyesha jinsi mchoro unavyoelezea pale juu.
Yaani japo mwanadamu ameonekana ni mdogo;lakini mbele za Mungu yeye ana
nafasi ya juu sana katika dunia hii.Mchoro huu ni baada ya Mungu kuumba dunia na kumweka mwanadamu ndani ya
dunia.
Mwanzo
.3 -Inatuonyesha kilichotokea ndani ya Bustani ya edeni–kama
nilivyokuambia kuwa shetani tayari alishakuwepo ndani ya dunia –na wala
hakufurahia hata kidogo nafasi aliyopewa mwanadamu – na vile vile hakuwa
tayari kuwa chini(kutawaliwa)ya
mwanadamu .
Kumbuka kuwa wakati Mungu anampa Adam maagizo ya kutokula matunda ya mti
wakatikati wa ujuzi wa mema na mabaya, Hawa/Eva alikuwa bado hajaumbwa-[Mwanzo.2:16-17,18-25].Kwa hiyo wakati
Mungu anatoa hayo maagizo shetani alikuwa anasikia maana alikuwepo.Na
yeye(shetani) alikuwa anajua kuwa Eva hakuwepo wakati Mungu akitoa maagizo
hayo,ila Eva alipata kujua hayo kutoka kwa Adam,Kwa hiyo alitumia nafasi hiyo
kutunga hila ya kumdanganya nayo mwanadamu ili yeye aipate hiyo nafasi ya
utawala wa Dunia hii.
Shetani alijua fika kuwa Mungu aliwaambia wasile matunda ya mti wa mema
na mabaya; ila alitumia maneno haya ya hila“ati hivi ndivyo alivyosema Mungu msile
matunda ya miti yote bustanini? …hakika hamtakufa…mtakuwa kama Mungu”
kwa lengo la kuwadanganya na kuwaingiza katika dhambi ya uhasi ambayo na yeye
aliifanya kule mbinguni akatupwa chini-[Isaya.14:13-14].
Mwanzo 3:1-4.Kitendo cha
Eva kuyaamini maneno ya shetani ni kwasababu alisikia kuwa akila hayo matunda
na yeye atakuwa kama Mungu,kwa hiyo na yeye alikuwa anataka awe kama Mungu,kama
vilevile shetani naye alivyotaka kumpindua Mungu ili yeye ndiye awe Mungu m
kuu,matokeo yake akatupwa chini.
Sasa matokeo ya dhambi waliyofanya
Adam na Hawa kulibadilisha muonekano wa ule mchoro wa pale juu wa utawala wa Dunia
hii - Dhambi ile, ilimpa shetani nafasi
ya kumiliki na kutawala Dunia hii badala ya
mwanadamu. Hata ule mchoro nao ukabadilika. Na ukawa kama hivi:-
MUNGU
BABA + MWANA+ ROHO MTAKATIFU
|
SHETANI
|
MALAIKA
|
↓
MWANADAMU
MME + MKE
|
Na kwasababu hiyo basi; dhambi hiyo ikasababisha mwanadamu kuwa chini ya
shetani na malaika pia –na ndio maana, [Yuda
1:9]
″…….lakini mikaeli malaika mkuu…hakuthubutu
kumshitaki (shetani)……Bali alisema Bwana na akukemee″.
Maneno haya ya malaika mikaeli yanaonyesha dhahiri effect(matokeo) ya dhambi iliyotokea bustanini kiasi kwamba malaika
hawakuwa na uwezo wa kumkemea shetani – kwa nini?_____Jibu ni kwa sababu
shetani ndiye amechukua ile nafasi ya mwanadamu kama mchoro unavyoonyesha hapo
juu.
Kwa hiyo baada ya mwanadamu kupoteza nafasi aliyopewa na Mungu ya
kutawala dunia hii,ilimlazimu Mungu atafute njia ya kumsaidia mwanadanu ili
aweze kurudi kwenye nafasi yake ya mwanzoni.Maana alishapoteza baada ya kutenda
dhambi na ndio maana Mungu alipomtembelea bustanini aliita akisema Adam,Adam
uko wapi? Maana yake Mungu alikuta kitu kingine(shetani) kwenye nafasi ya Adam.
Hivyo Mungu akaanza kuweka mipango ya kumkomboa mwanadamu kutoka
mikononi mwa shetani na amrudishe kwenye postion(nafasi) yake ya mwanzo.Mpango
kwa lugha ya kingereza unaitwa “plan” ukisoma kamusi ya kingereza
ya Oxford toleo la 7 inaelezea vizuri maana ya plan(mpango).Na katika kupanga
mipango ili kufikia kusudio fulani, huwa ni lazima uwe na plan A na plan B.Hii
inamaanisha kuwa plan A ikifeli(shindwa) plan B inaingizwa kazini.Sasa plan B
kwa jina lingine inajulikana kama “MASTER PLAN” na mfano mzuri wa plan
B ni sawasawa na kazi ya gear(gia) namba moja ya kwenye gari na kwa kawaida
sikuzote inapofika kwenye mwinuko mkali,gia zingine zitashindwa lakini namba
moja yenyewe haitashindwa labda hilo gari liwe ni bovu.
Sasa usije ukafikiri kuwa nafundisha
maswala udereva wa magari!
Hapana!.Ninachotaka hapa ni ili uelewe vizuri plan(mpango)A wa Mungu na plan
B(Master plan) ya Mungu katika kumrudishia mwanadamu utawala wa dunia hii.
Sasa embu tuangalie plan
zote mbili jinsi zilivyofanya kazi:-
PLAN
A:MPANGO “A” WA MUNGU KUMRUDISHIA
MWANADAMU UTAWALA WA DUNIA HII.
Baada ya Mungu kuona kuwa Mwanadam
ameshapoteza nafasi aliyokuwa amempa,ikabidi Mungu aingize plan A kazini,na
mpango huu aliuanzia kwa Ibraham-Isaka-Yakobo→Musa→Daudi.Kipindi cha Musa Mungu
alimwagiza Musa ajenge hema na aweke makuhani na damu ya makondoo na mafahali
ilitumika katika kuwapatanisha wanadamu na Mungu na kuwafanya wapate nafasi ya
kutawala tena-(Kutoka.25,27,27,28).
Lakini
pamoja na hayo yote mpango huu(plan A) haukuweza kufanikisha lile kusudi la
Mungu la kumrudishia mwanadamu nafasi aliyoipoteza,damu za wanyama hazikuweza
kumbadilisha mtu kutoka kwenye dhambi alizokuwa nazo mfano:mtu mlevi au mzinzi
kuachana na tabia hizo alizonazo,Sio hivyo tu bali damu hizo za makondoo na
mafahali hazikuwa na uwezo wa kumshinda shetani; shetani aliendelea kujitapa na
kujiita yeye ndiye mungu wa dunia hii.Hata yale matokeo mabaya yaliyosababishwa
na dhambi ya bustanini,hii kama vile magonjwa(ukoma)- plan A, ya damu za
mafahali na makondoo haikuweza kuondoa magonjwa hayo, watu waliendelea kuteseka
na magonjwa yao bila msaada wowote na ikafikia hatua hata yaw engine kutengwa
na jamii ili wasiwaambukize wengine.[2falme.7:3].
Kwa hiyo kila
mtu alipokuwa akitenda dhambi ilimbidi atafute kondoo wa kumpeleka kwa kuhani
ili akasamehewe dhambi zake[Lawi.5:1-10].Kwa
hiyo kila siku damu za makondoo na mafahali zilikuwa zikimwagika hekaluni;
lakini hata hivyo plan “A” haikufanikiwa.Na katika plan hii Mungu aliwatuma
manabii mbalimbali wengine waliuawa na kuteswa na Shetani akafikiri kuwa sasa
yeye ameshindikana au amekuwa chronic.
Hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kukemea pepo kwasababu damu hizi za wanyama hazikuwa na uwezo huo.
SEHEMU YA PILI
PLAN B(MASTER PLAN) -UJIO WA YESU NA MATOKEO YA KIFO
CHAKE.
Baada ya
plan A kufeli Mungu akaamua aingize plan B kazini,Plan B hiyo ni Yesu-na mwili
wake(kanisa) ambalo yeye mwenyewe amesema kwamba malango ya kuzimu
hayatalishinda kanisa la Mungu.Na kama nilivyokuambia Hapo mwanzo kuwa plan B
ndio “master
plan” na kwa kawaida sikuzote plan B (master plan) huwa yenyewe
haishindwi; yaani yenyewe ndio solution ya kila kitu.Kwa hiyo alichokifanya
Mungu ni kuamua kuja mwenyewe ulimwenguni kumshughulikia shetani na kumpokonya
ule ufalme aliouiba;na kumrudishia binadamu utawala wa dunia hii.Na ndio maana
Yesu akaamua kuuvua utukufu wake na kuvaa utu ili tu aweze kutukomboa.Kwa
sababu asingeweza kutukomboa bila ya yeye kuvaa ubinadamu.Kwa sababu ukombozi
wetu ulihitaji Damu yenye nguvu kuliko ile ya mafahali na makondoo iliyotolewa
enzi za agano la kale ambayo haikuweza kumsaidia mwanadam kushinda dhambi na
shetani[Ebra.9:22b] inasema “na
pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo(la dhambi)”
Pia kuja kwake(Yesu) kwa namna
ya mwili ni ili awe kielelezo cha sisi kuiga na kuishi maisha aliyoyaishi hapa
duniani.Na ndio maana alikuja kwa namna ya mwili ili aweze kutuhubiria, kwa
hiyo alipita kijiji baada ya kijiji akihubiri.Embu fikiria kwamba; je angekuja
kwa namna ya kiungu ingekuwaje[kut.20:18-19]
“…..na watu walipoona hayo wakatetemeka
wakasimama mbali,…Musa sema nasi wewe ,nasi tutasikia,bali Mungu asiseme nasi,
tusije tukafa”
Kwa hiyo Mungu akaamua kuuvaa
mwili ili aje atukomboe [filp.2:5-11,ebra.2:17;4:15]
Hivyo ujio wa Yesu ulikuwa na kusudi la kutukomboa na kuturudishia ufalme na
nafasi nyingine ya upatanisho(ukuhani).Huduma ya upatanisho iko ndani ya huduma
ya ukuhani-[kut.32:30;2kor.5:18-19].Sasa
fuatana nami,nitakueleza kazi ya huduma hii ya upatanisho ndani ya ukuhani
inavyotakiwa kufanya kazi nyakati hizi za leo-[Ufu.59-10] inasema kwamba tumenunuliwa kwa damu ya Yesu na
tukafanywa kuwa makuhani na ufalme kwa ajili ya Mungu wetu.[1petro.2:5,9-10].Kwa hiyo alichofanya
Yesu ni kumwaga damu yake ambayo kwa hiyo damu sisi tumenunuliwa na baada ya
kutununua akaturudishia ule ufalme tuliopokonywa na ibilisi hapo mwanzo kwa
njia ya dhambi; na ili shetani asije akautwaa tena huo ufalme,Yesu aliamua
kutuongezea huduma ya ukuhani kwa lengo la kulinda nafasi ya ufalme isije
ikapotea tena.
Huduma ya
ufalme na ukuhani ni nafasi ambazo zinakwenda kwa pamoja na wala huwezi
kuzitenganisha.Hivyo bila ukuhani, ufalme wetu hauwezi kuthibitika.Yaani ni
sawasawa na mfalme asiye na walinzi au nchi isiyo na jeshi;na kwa namna hiyo
kamwe ufalme huo au nchi ya namna hiyo ni rahisi sana kuvamiwa na kutekwa na
kumilikiwa na maadui.Kwa hiyo huduma hii ya ukuhani ni ya muhimu sana katika
kuhakikisha kuwa ufalme wako haupotei na wala adui hapati nafasi juu ya eneo
unalotawala.Kumbuka kuwa wewe mtu uliyeokoka;Mungu anakutazama wewe kama mfalme
wa eneo uliloko,hivyo na wewe unatakiwa ujione hivyohivyo kama jinsi vile Mungu
anavyokuona na sio vinginevyo. Sasa kabla hatujaenda kuangalia nini maana ya
kuwa mfalme,naomba tuangalie kwanza aina mbili za falme,katika ulimwengu wa
roho.
Katika
ulimwengu wa roho kuna ufalme wa nuru au wa Mungu na ufalme
wa pili ni ufalme wa giza(shetani).Falme zote hizi mbili zinatafuta nafasi ya
kuimiliki dunia hii.Na ili kuimiliki dunia hii ni lazima mwanadamu
ahusishwe.Kwa hiyo ufalme wa Mungu unatafuta watu ambao watasimama kwa niaba ya
ufalme wa Mungu ili waimiliki dunia-na mmoja wa watu hao ambao ufalme wa Mungu
unawatafuta ni wewe mpendwa uliyeokoka.Sasa shetani naye anawatafuta watu
watakaolisimamia kusudi lake,ili ufalme wake ufanikiwe…kipengele hiki cha falme
mbili kitaedelea sehemu ya tatu(3).
Kwa hiyo ujio
wa Yesu ulileta mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu wa roho.Na kitu
alichokifanya Yesu ni kumnyang’anya shetani ile nafasi (ufalme/utawala) aliyoiiba kwa hila pale
bustanini Edeni –[Mwanzo .3 ]na
kumrudishia mwanadamu.kwa hiyo Yesu alimtoa shetani katika hiyo nafasi alafu
akatuchukua na kuturudishia ile nafasi yetu ambayo Mungu alikusudia tuwe nayo
tokea awali,yaani nafasi ya kumiliki dunia-[Mwanzo 1:28].
Ufunuo 5:9-10.inasema
hivi:-
″…………kwa
kuwa ulichinjwa ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na
jamaa na Taifa (10)ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu;nao
wanamiliki juu ya nchi”.
Kitu
alichokifanya Yesu ni kutukomboa kwa damu yake;alafu akaturudisha kwenye nafasi
yetu ambayo Mungu alikusudia tuwe nayo tokea mwanzo wa uumbaji wake Mungu –
yaani nafasi ya ufalme ya kumiliki na kutawala.[mwanzo.1:26-28].
KUWA MFALME MAANA YAKE NI NINI?
Kuwa mfalme maana yake wewe ndio mtawala wa eneo uliloko;iwe ni familia
,mji ,shule,kanisa,nchi nk.Na hii inamaanisha kuwa watu wote wa eneo hilo wako
chini ya utawala wako,yaani ni raia wako; iwe ni ndugu zako au si ndugu
zako.Sasa ni lazima ufahamu kuwa kila ufalme una mipaka yake na mipaka hiyo
inaheshimiwa na kutambulika kisheria na kimataifa kuwa inamilikiwa na mfalme
fulani.Na ili ufalme wako uwe imara ni
lazima:-
i)Uwe na mipaka yako inayotambuilika(miliki ardhi) kisheria.
ii)Uwe na watu na pia watu hao
uwe una uwezo wa kuwasaidia kupata mahitaji yao ya msingi.
iii)Miliki Anga+maji.
Hii inamaanisha
kuwa lazima kuwe na ulinzi katika mipaka ya ardhi na pia juu ya mipaka ya anga
lako.Kwa nini kuwe na ulinzi kwenye mipaka ya ufalme wako? Jibu lake ni
hili-kwa nini Tanzania ina jeshi la ardhini,la maji na la anga?Sasa nakupa
homework ya kujua kwa nini kuwe na jeshi la nchi kavu(ardhi),la maji na la anga
katika Tanzania-ukipata jibu lake utatambua umuhimu wa kuwa na maombi ya
kuombea anga,ardhi,maji na watu.Nchi ya Tanzania ina mipaka yake ya anga ambayo
sio rahisi nchi nyingine iingilie bila ya idhini ya Tanzania.Na ndio maana sio
rahisi uone ndege ya jeshi la Kenya ikiruka kwenye anga la Tanzania bila idhini
ya Tanzania,ikitokea hivyo ujue huko niuchokozi wa vita.Sasa usifikiri kuwa
nakufundisha siasa, hapana!, ila ninataka kupitia mifano hiyo ujue jinsi
ulimwengu wa roho unavyofanya kazi.Hata Yesu alitumia mifano katika mafundisho
yake.Hivyo wewe kama mfalme ni lazima utawale na kumiliki ardhi,watu wake na
anga la sehemu unakoishi ili mambo yako na mipango yako iweze fanikiwa(yaani kuanzia sasa anza kujiona wewe
ni mfalme wa Eneo uliloko;
yaani familia yako/kanisa /mji/nchi nk. [Daniel.10:12-13;20].
KWA NINI WEWE NA SIO MALAIKA?
Huwa najiulizaga swali hili kwamba ni kwa nini Mungu ametuchagua sisi
kuwa watawala wa dunia hii,kwa nini hajawachagua malaika kuchukua nafasi
hii?.Kwa kweli Mungu amekuheshimu sana
akakupa nafasi hiyo kwa sababu ya
makusudi yake ,yaani Mungu alikusudia wewe uwe mungu wa dunia hii. Sasa ujio wa
Yesu ulikuwa ni kuja kutimiza kile ambacho Mungu alikukusudia-Yohana.10:34-36.
“Yesu akawajibu ,Je haikuandikwa katika
korati yenu ya kwamba ,mimi nimesema ndinyi miungu?………….″ [source-Zab 82:6]
v Kwa hiyo
yesu alipokuja alibadilisha mfumo wa utawala wa dunia hii.ukawa kama uonekanavyo hapa chini.
MUNGU
BABA + MWANA+ ROHO MTAKATIFU
|
↓
MWANADAMU
(ALIYEOKOKA)
|
↓
MALAIKA
|
Inaendelea uk. Ujao…..
SHETANI
|
↓
WAOVU(watu)
|
Kwa hiyo Yesu alituhamisha
kutoka katika ufalme wa giza
(kutawaliwa na shetani)na kutuleta katika ufalme wa pendo lake.
[ Epheso 2:6]″……..akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika kristo Yesu″.
SASA ANZA KUJITAMBUA KUWA :-
Ø Wewe ni mfalme na kuhani wa Eneo unaloishi na wewe
ndiwe unayetakiwa umiliki hilo eneo.Ufu.5:9-10.kutoka19:6, 1petro 2:5,9-10.
Ø Wewe ni kiumbe kipya ndani ya kristo. 2korinto 5:17
Ø Wewe unazo funguo za ufalme wa mbinguni. mathayo 16:18-19;mathayo 18:18
Jambo lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa kule mbinguni
.Kwa hiyo wewe ndio mwenye maamuzi ya
mwisho ya Eneo unaloishi.unaweza ukaamua shetani aendelee kutawala au
asiendelee.
Ø wewe ni rungu na silaha za vita za Bwana –Jeremia 51:20-23.
-kazi yako kama rungu ni kuvunjavunja kazi za ibilisi-hiyo ndiyo kazi
aliyokupa Yesu . Yohana.17:15,
-wewe upo hai na umeokoka kwa sababu ya makusudi fulani ndio maana yesu
ameomba kwamba tusiondoke katika ulimwengu huu.
1Yohana 3:8″……..kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa
ili azivunje kazi za ibilisi ″.
Hiyo
pia ndiyo kazi uliyopewa ndio maana anasema wewe u rungu langu na silaha
zangu za vita.
Ø Fahamu udhaifu wako na umkabidhi Yesu udhaifu wako.
-[2korintho.12:7-10] Mungu au
Yesu wetu huwa anatafuta madhaifu yetu ili adhihirishe uwezo na ukuu wake
kwetu.Wakati huo huo Shetani naye anatafuta udhaifu wako ili autumie kukumaliza
nao.Hivyo ni lazima utambue udhaifu wako na uukabidhi kwa Mungu kabla shetani
haujautumia kukuangamiza nao.
Fahamu kuwa hakuna
kitu kibaya kama adui yako kujua madhaifu yako,ni hatari sana!.Unajua shetani
aliufahamu udhaifu wa petro kuwa ni muongeaji sana[Mathayo.16:22-23].Alifahamu
udhaifu wa Yuda kuwa ni mpenda pesa[Yohana.12:4-6].Aliufahamu udhaifu wa
Daudi,wa Suleiman nk.Na hata wakwako anaufahamu;sasa cha kukusaidia ni kwamba
mkabidhi Mungu madhaifu yako yote kuanzia leo.Pengine udhaifu wako ni ugonjwa
fulani hakikisha unaukabidhi kwa Yesu kama Paulo
alivyofanya[2korintho.12:7-10].Kumbuka kuwa kabla ya Paulo hajaufahamu udhaifu
wake na kuukabidhi kwa Bwana,shetani aliutumia udhaifu huo kumtesa nao Paulo[soma vizuri 2korintho.12:7-10].Embu
fikiria kuwa kila unapotaka kuanza maombi unaanza kusikia maumivu au
kuumwa;sasa kama hufahamu huo ndio mwiba(udhaifu)wako ambao shetani anautumia
kukutesa nao ili usiweze kupambana na yeye.
Ø Fahamu kuwa dhambi ndiyo mlango wa shetani kuingilia
sehemu au Eneo fulani la maisha
yako .Mwanzo.3:-
Ø Fahamu kuwa toba ya Damu ya Yesu ni muhimu sana kila siku
kwa ajili ya maombi yako juu ya
mji/kanisa na familia yako hivyo jizoeze kuitumia kila siku.
Ø Kila mahali utapokanyaga kwa unyayo wa miguu yako, Bwana
amekupa wewe kumiliki eneo hilo.Yoshua
1:3
NB:Haya
ni mambo ya msingi sana ya kuyazingatia kabla haujaingia kwenye vita ya rohoni
dhidi ya shetani; kuna mengine mengi ya kujua
kupitia Roho mtakatifu na kusoma kwako neno la Mungu.
v Sasa baada
ya kujitambua/fahamu wewe mwenyewe,pia tambua
au fahamu haya yafuatayo:-
i)Fahamu ni nani unayepambana naye(yaani adui yako)[efeso.6:12]
ii)Ni silaha gani
anazotumia,adui yako
iii)Mbinu gani anazitumia
kukushinda(hila)[2korintho.2:11,Mwanzo.3].
Siri kubwa ya
ushindi wa shetani kwetu ni dhambi;na pasipokuwa na dhambi si rahisi shetani
kupata nafasi; kwa hiyo dhambi ni mlango mkubwa wa shetani kuingia sehemu
yeyote.Ukiona mji unamilikiwa na adui ujue kuwa kuna dhambi ilifanyika
ikamfungulia shetani mlango wa kutawala.Mfano
mzuri ni wa Ayubu; shetani alitafuta mlango wa kumvamia ayubu lakini Ayubu
alikuwa akifanya maombi ya toba kila siku kwa ajili ya watoto wake na kwa ajili
yake yeye mwenyewe.[Ayubu.1:5-10a].Toba
ya Ayubu ilimtengenezea wigo/ukuta wa moto ambao shetani alishindwa kuuvuka.[Zekaria.2:5].
SEHEMU YA TATU.
Aina za falme 2 katika
ulimwengu wa roho (kutoka sehem ya 2).
1:UFALME WA MUNGU(NURU)
2:UFALME WA SHETANI(GIZA).
Kama nilivyotangulia kusema
katika sahemu ya pili kwamba zko falme mbili katika ulimwengu wa roho.Na ili
falme hizi zote mbili ziweze kuwa na full control (umiliki)wa Eneo husika ni
lazima wafanikiwe kumiliki Anga,Ardhi na watu.
Note vitu hivi:-
a)–ufalme usio na watu sio ufalme,
b)–ufalme usio na mipaka yake sio ufalme,
c)–ufalme usiokuwa na umiliki wa anga sio
ufalme.
Kwa hiyo ili
falme moja kati ya hizi ziweze kuthibitika
ni lazima zimiliki Anga,Ardhi na watu eneo husika.Hii inamaanisha kuwa ili
shetani aweze kuwa na full control ya Eneo husika ni lazima amiliki anga ,Ardhi
na watu.Anapofanikiwa kufanya hivyo; ufalme wake unathibitika,na yeye ndio
anakuwa mfalme wa eneo hilo.
Sehemu ya anga
ndiko shetani anapowaweka wakuu wake wa utawala wake yaani wakuu wa
giza-mf.belizebuli.(Biblia ya kiingereza inasema "Evil spirits who
overrules the kingdom…..)roho zitawalazo.marko.3:27,mat.12:29.Yesu
anawatambulisha kama “mtu mwenye nguvu”.Ukitaka kufahamu ni jinsi gani hao
wakuu walivyo fananisha na jinsi lilivyo jeshi letu(ranking);huwa kuna amiri
jeshi mkuu(rais),mkuu wa majeshi,majenerali,luten,kapten nk.Kwa sababu mimi si
mwanajeshi,nadhani ni vyema ukimpata mwanajeshi yeyote yeye anaweza kukuelezea
zaidi mtiririko mzuri wa hierarchy ya jeshi.
Hii inamaanisha kuwa
katika kila mji nchi,familia,kanisa nk.shetani ameweka wakuu wake(mf.jinsi rais
wa nchi anavyoweka wakuu wa mkoa katika kila mkoa)-kumbuka kuwa nimekuambia kuwa
wakuu hao (wa anga) ni ile roho au zile
roho zinazotawala eneo husika,sanasana ile iliyoanza kuwepo kwenye eneo hilo.
-Kwa hiyo ufalme
wowote kati ya hizi mbili unapofanikiwa kuteka eneo lolote basi jua kuwa
Anga,Ardhi na Watu wote watamilkiwa na ufalme huo.
Daniel.10:12-13,20. Kufanikiwa kwa Daniel na wale wenzake ni
kutokana na maombi yao juu ya mji na nchi waliyokuwa wanaishi(Babeli).Daniel
alipata kibali mbele ya mfalme wa babeli,lakini viongozi wengine wa taifa lile
hawakufurahia na ndio maana walitunga hila ya kumuua ili wao wapate nafasi ile[Daniel.6].
Esta.3- Hamani alitaka kuwau wayahudi wote kwasababu tu alichukia
kumwona mordekai na esta katika uongozi, kilichowaokoa wayahudi ni maombi
yao.Wayahudi walichukiwa kwasababu sheria zao zilikuwa zinapingana na sheria za
miungu ya akina hamani.
Katika nyakati za leo,kama
tutashindwa kuombea miji,nchi na maeneo tunayoishi, itakuwa ni vigumu sana
kupata viongozi wazuri.Kwasababu asilimia kubwa ya maeneo tunayoishi yako chini
ya utawala wa giza.Na utawala wa giza wakiwemo wachawi hawako tayari kuona miji
au maeneo yao yanamilikiwa na viongozi kutoka kambi ya Adui(ukristo(waliookoka).Maana
wanajua kuwa kiongozi akiwa ni wa kutoka kambi ya upinzani(ukristo) basi
utawala wao uta pata shida. NB:Tatizo
kubwa walilonalo wanamaombi wengi katika kuomba kwa ajili ya Mungu kutupa
viongozi wazuri , ni kwamba wanasubiria mpaka vyama vya siasa vimewachagulia
viongozi, ndio wao wanaanza kumwomba
Mungu awape kiongozi mzuri kati ya wale waliochaguliwa na chama.Kumbuka kuwa
chama hakina Mungu na wazee wengi wa vyama hawana Mungu na ndio wao wanaopanga
mwaka ujao raisi awe nani hata kama ni mbaya wanachojali wao ni masilahi yao na
ya chama nasio ya nchi.Kama tunataka kiongozi mzuri katika nchi yetu ya
Tanzania au katika miji tunayoishi, ni lazima tuanze kuwaombea kuanzia leo
kabla ya mwaka 2015.
Utatambuaje jina la mkuu wa giza(anga-mtu mwenye nguvu) anayemiliki eneo unaloishi?
·
Angalia ni
matendo gani ya giza yametawala eneo hilo.
Kwa mfano:utakuta katika
mji Fulani uchawi ndio umeenea sana na hata habari zinazozungumziwa ni uchawi
na uganga;wakati mwingine utakuta mji unasifika kwa vitendo vya
mauaji,uzinzi/uasherati,ajali mafarakano na ulevi na vifo vya kiroho.Kwa
namna nyingine unaweza ukatambua jina la mkuu wa giza(anga) wa eneo unaloishi
kwa kuangalia ule uovu ulioanza kabla ya maovu mengine ,kumbuka kuwa kila uovu unaotendeka kuna pepo nyuma yake;uzinzi
unasababishwa na pepo la uzinzi.
-Mara
nyngi unapokuta sehemu kuna mafarakano ujue umesababishwa na mapepo kama ya kiburi,majivuno,uchawi
na uhasi.
v [Daniel.10:12-13;20].
Kitabu hiki cha
danieli kinatuonyesha kuwa aliyekuwa anamiliki anga la uajemi na uyunani ni
ufalme wa giza.Na ndio maana wakina Daniel na wenzake walikuwa wakipigwa vita
kwa sababu walikuwa wanaenda kinyume na ufalme uliokuwa unatawala anga la
uajemi-babeli(yaani ufalme wa giza).Na ndio maana wakina meshack,shedrack na
abedinego walitupwa kwenye tanuru la moto na Daniel akatupwa kwenye tundu la
simba.
Na kwa kwaida siku
zote shetani anawatumia wanadamu wenzetu katika kukamilisha kazi zake hapa
duniani-mf.kule Babeli-aliwatumia viongozi.Na ndio maana mtume Paulo anatuambia
kuwa tuombee wale wanaotutawala(viongozi).
Kwa hiyo ili ufanikiwe
na kazi ya Mungu ifanikiwe ni lazima ujifunze kuombea mji unaoishi;kinyume na
hapo ni kutokufanikiwa na kupigwa vita kila siku.Kwa hiyo usipomiliki anga na
ardhi,kwa kweli utakosa Breakthrough(mpenyo) katika maombi yako na hata kwenye
mafaniko kimaisha,kimasomo,kibiashara na kwenye huduma yako[kiroho na
kimwili].Pia fahamu kuwa mfalme humiliki kwa maneno yake –yeye huwa anaagiza tu
kwamba ifanyike alafu inafanyika.Pia wafalme kipindi cha agano la kale
walikwenda vitani;kwa hiyo nawewe unatakiwa uingie vitani inapobidi.[1Nyak.20:1, 2Nyak.20:20-23]
Nb: Kufanikiwa kwa Mji unaoishi ndipo na wewe utakapofanikiwa kwa
hiyo usiache kuuombea,na kuutakia amani mji huo unaoishi.
Yeremia.29:5-7 inasema
hivi “Jengeni
nyumba mkakae humo….kautakieni amani mji ule….mkauombee Kwa Bwana, Kwa maana
katika amani ya mji huo ninyi mtapata amani”
Wewe kama
mfalme wa eneo unaloishi ni lazima uhakikishe kunakuwa na usalama juu ya watu
wako(raia) aliokupa Bwana ,pia uhakikishe kuna ulinzi wa kutosha kwenye
anga,ardhini na majini(toba ya damu ya Yesu kila siku juu ya maeneo
hayo).Kumbuka kuwa mwanzo nilikuambia kuwa huduma hii ya ufalme haiendi au haijitegemei peke yake bali inategemea
huduma ya ukuhani yenye
upatanisho ndani yake na katika kuhakikisha ulinzi wa maeneo hayo manne yaani
ardhi,anga,watu na maji na maeneo unayoishi, ni lazima huduma ya ukuhani iingie
kazini.
KAZI
YA UKUHANI :
·
Kufanya maombi ya toba kwa ajili ya
ardhi,anga,maji(bahari,mito na maziwa) pamoja na watu,kuta na malango ili
kutakasa.[Neh.12:30]
·
Kufanya maombi ya upatanisho-ili kurejesha mahusiano ya
mwanzo yaliyopotea baina ya Mungu na watu wake na eneo husika.[kut.32:32]
·
Kutengeneza mahali palipobomoka na kuzuia hasira ya Bwana
kwa njia ya Toba ya Damu ya Yesu.[Eze.22:30-31]
-Kusimama mahali
palipomoka maana yake ni kusimama katikati ya.Maana yake unasimama katikati ya
Mungu na ndugu zako au mtu mwingine ambaye unataka kumwombea toba au maombi
yoyote na pia kusimama katikati ya Mungu na mji au nchi yako,mfano mzuri ni
ibrahim[Mwanzo.18,19].Kwa hiyo Mungu
amekuinua wewe kama mwombezi kwa ajili ya mji,kanisa,familia na nchi uliyoko na
hata biashara za eneo hilo.
·
Wewe kama kuhani unapoombea mji au nchi(ardhi,anga,na watu)
ni lazima ujue jinsi ya kuwaombea watu hao na mji huo,yaani omba kama mama au
mzazi anayemwombea mtoto wake(omba kama unajiombea mwenyewe).Na mfano mzuri ni
maombi ya Musa naya Daniel[Daniel.9:4-19].
Maana Mungu anamtafuta mtu wa kufanya maombi ya kikuhani kama ya Daniel.[Eze.22:30-31],au ya Musa[Kut. 32:32].
Pia fahamu kuwa
unapookoka unakuwa mfalme na kuhani maana yake ndugu zako wote wako chini yako
na pia mji na watu walioko ndani yake wote wapo chini yako.Wewe ndio mwenye
final say & final decision(maamuzi ya mwisho).Maana yake ukisema “No”
inakuwa “No” ukisema “Yes” inakuwa “Yes” ndio maana Mungu akakupa funguo za
ufalme wa mbinguni [Mathayo
16:18-19].
Wewe kama kuhani,unayo
nafasi mbele za bwana ya kumwomba Mungu kwamba Mungu awaokoe ndugu zako,yaani
wasife katika dhambi na Mungu akafanya hivyo.Mfano,Ibrahim alimwomba Mungu
amwokoe ndugu yake Lutu asipatwe na ile adhabu yamoto juu ya sodoma na gomora.[Mwanzo.18,19].Pia Musa aliomba Mungu
asiwaangamize waisrael na Mungu akamsikia.pia Mungu anakuheshimu sana unapokuwa
kuhani na mlinzi. [Eze.3:17-21].
Watu wengi wamekuwa
wakifa kwa magonjwa,na wengine kwa ajali na huwa wengi wanakufa wakiwa na
dhambi na direct wanakwenda motoni.Hii ni kwasababu makuhani na
walinzi(wanamaombi) wameshindwa kusimama katika nafasi zao.
UTAJUAJE KUWA ANGA LINAMILKIWA NA ADUI?
I: Upinzani mkubwa katika
kumtumikia Mungu.
Utakuta kila
unapojaribu kumtumikia Mungu;ndugu,jamii,bosi
kazini, wote wanakupiga vita.Marko.5:1;-katika sura hii unaweza
ukadhani kuwa ni wale watu ndio walioamua kumfukuza Yesu katika mji wao,la hasha hapana.Bali ni
kwamba mji ule na anga lake na watu wake walikuwa wanatawaliwa na kumilikiwa na
adui na ndio maana badala ya kufurahia muujiza ule na kumkaribisha Yesu kwa
ajili ya muujiza alioufanya kwa yule mtu aliyekuwa ameshindikana kwa muda mrefu
wao wakaamua kumfukuza kwenye kijiji chao.
Matendo.4:1-5,18.
II:
Ugumu wa kuomba (mpenyo wa maombi
unakuwa mdogo)
Mara nyingi utajikuta
unashindwa kuomba; unapofika muda wa maombi unaanza kupatwa na usingizi mzito
na muda mwingine unakuwa unapiga miayo tu.
III:Vifo vingi vya kiroho na vya kimwili.
Watu wengi wanaokoka lakini
baada ya muda mchache wote wanarudi nyuma.
IV: Kupoa kiroho kwa watumishi na
wanamaombi wengi.
-Utakuta watu walikuwa na kasi
na juhudi katika wokovu lakini baada ya muda wanakuwa vuguvugu.ufunuo.3:14-21
V: Kuenea kwa mafarakano kwenye kanisa,
familia,miji,nchi n.k
-Makanisa mengi leo hii
yamejawa na migogoro; wachungaji dhidi ya wazee wa kanisa wanagombana n.k
VI: kushamiri kwa matendo ya giza(maovu)
-Kama anga linamilikiwa na
adui si ajabu kukuta uzinzi, uasherati, ujambazi, uchawi na kila
tendo chafu na ovu la giza.Yote hiyo ni kwasababu tayari mji huo
umekuwa makazi ya mapepo.
Ufunuo.18:2 “…umeanguka,umeanguka Babeli ule mkuu;umekuwa maskani ya
mashetani,na ngome ya kila roho mchafu,na kila ndege mchafu mwenye kuchukiza”
-Hizi ni baadhi ya alama
chache tu za kujua kama Anga linatawaliwa na Adui au la!
KWA NINI UMILIKI MJI(ARDHI,WATU NA ANGA LAKE?
I: Lazima umiliki mji,anga
n.k, kwa sababu wewe ni mfalme tena ni kuhani wa Bwana.Na kama
wewe ni mfalme na kuhani wa Bwana kama biblia isemavyo katika kitabu cha;Ufunuo.5:9-10,Basi ujue kuna eneo ambalo wewe unatakiwa ulitawale
kama mfalme wa eneo hilo.
Na ili ufalme wako uweze
kuwa na nguvu ni lazima umiliki Anga,Ardhi,na Watu.Kinyume na hapo ufalme wako
hauwezi kuthibitika na ufalme huo uko mashakani-wewe unafikiri ni kwasababu
gani Tanzania tuna jeshi la Anga,nchi kavu,majini n.k- Jibu ni kwasababu ya
kulinda Anga,ardhi,maji na raia wa Tanzania-na ndio maana ni lazima ujizoeze kuombea Anga,Ardhi,maji na watu wa
sehemu unakoishi.
Usipoombea mji na Anga
unakoishi basi jua kuwa utakuwa kila siku unapigwa vita na kukutana na vikwazo
kwenye kumtumikia kwako Mungu, kwenye uchumi, afya yako,na biashara yako
n.k.Yesu alisema kesheni muombe msije mkaingia majaribuni[Mathayo.26:41].
Hivyo kama unataka
breakthrough (mpenyo) kwenye maisha yako ya kiroho na ya kimwili ni lazima
umiliki mji,watu na anga la eneo unaloishi;ukishindwa kufanya hivyo basi jua
utapata vita kubwa sana,kiroho na kimwili.
II:Kwasababu kufanikiwa kwa mji
unaoishi ndipo na wewe utakapofanikiwa kiroho na kimwili.Yeremia.29:5-7.
-unapoombea mji unaoishi
utasababisha kuuepushia mji huo na maangamizi na majanga kama vile
ajali,vita,mafuriko,moto,tsunami n.k
·
Ezekiel.22:30,
Bwana anamtafuta mtu atakaye simama ili kuuombea mji ili hasira ya bwana
isimwagwe kwenye mji.ukisoma vizuri sura hii ya ezekiel.22 utaona kuwa kinachosababisha Bwana atake kumwaga
hasira yake ni kwa sababu ya maovu kama uzinzi, rushwa n.k
·
Isaya.62:6-7,Bwana
anasema kuwa ameweka walinzi juu ya mji wa yerusalemu.Pia katika mji unaoishi
Bwana ameweka walinzi na mmoja wapo akiwa
ni wewe.Na unapokubali kuwa mlinzi ni lazima uwe unaomba maombi haya “ufalme
wako na uje na mapenzi yako yatimizwe…”.Ufalme wake uje wapi?ni kwenye mji
unaoishi.
-Hii inamaanisha kuwa
unapoomba maombi haya ufalme wa Mungu unakuja na kumiliki na kutawala mji, anga
lake, na watu waishio ndani yake.
Lakini kabla ufalme wa
Mungu haujaja ni lazima utumie hiyo nafasi ya ukuhani uliyopewa kwa ajili ya kutengeneza na kutaarisha mazingira
ya ujio wa ufalme wa Mungu kwenye mji unaoishi.Yaani uachilie maombi ya toba ya Damu ya Yesu kwenye mji,ardhi yake,anga lake na
watu wake.
-Nehemia .12:30, inasema hivi; “Na makuhani na walawi wakajitakasa, wakawatakasa watu, malango na
kuta”
Toba yako ya mara kwa mara +
Maombi ya kuombea ufalme wa Mungu uje kwenye eneo unaloishi.Yatakufanya
umiliki mji na anga la eneo unaloishi.
III: Kwasababu sisi ni uzao wa
ibrahimu.
-Bwana alimwambia ibrahimu
kuwa wazao wako watamilki malango ya Adui zao na miji ya adui zao.Mwanzo.22:
SEHEMU
YA NNE(4):KANUNI…
JINSI YA KUTEKA NA KUANZA
KUMILIKI MJI NA ANGA AMBALO ADUI AMESHALISHIKILIA TAYARI.
·
Kwanza
fahamu jambo hili kuwa aliyeumba Dunia, mbingu (anga) na vyote vijazavyo ni
Mungu.Hii
inamaanisha kwamba hata mji unaokaa ni Mungu ndiye aliyeuumba, hata sehemu
anakoishi shetani ni Mungu (YESU) ndiye aliyeumba vyote hivyo.Yoh.1:1-5. “…..vyote vilifanyika kwa huyo,wala pasipo
yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika….”
-Kwa hiyo shetani
hakuumba chochote bali yeye aliumbwa tu.Zaidi sana alichokiumba yeye ni dhambi na maovu tu.Hivyo
unapoona anamiliki eneo fulani jua kuwa; kuna uhalali au kibali fulani
amekipata kutokana na dhambi na maovu yaliyotendwa na yanayotendwa na watu katika
mji husika(huo).
-Shetani ni mvamizi ni sawasawa na jinsi
wakoloni walivyofanya kwa waafrika, kwa kuwavamia na kuwatawala.Kwahiyo
unapoona shetani analimiliki eneo fulani jua kuwa ana haki/uhalali fulani
ameupata kutokana na maovu na madhambi yanayotendeka katika mji huo.Pengine ni
mazindiko yaliyofanywa na mababu,uzinzi,uchawi unaotendeka kila siku n.k.
·
Mathayo.4:8.
-Wewe unafikiri ujasiri
huo shetani aliutoa wapi wa kuthubutu kumwambia muumbaji wake(Yesu)[Yohana 1:1-5]kuwa akimsujudia yeye atampa mali zote za ulimwengu
huu.
-Shetani alipata uhalali wa
kumiliki Dunia hii baada ya dhambi ya akina Adamu na hawa.
-Ili sasa uweze
kulimilikiAnga sharti au kwanza ufanye toba ya Damu ya Yesu kwa ajili ya Eneo hilo.unapo
achilia maombi ya toba ya Damu ya Yesu, kwenye Eneo lako kinachotokea ni kwamba
ule uhalali wa shetani wa kumiliki hilo Eneo unaondolewa au unafutwa na damu ya
Yesu .Halleluya!.
Baada ya kufanya maombi ya
Toba ili kuliteka Eneo hilo ni lazima ujue jinsi ya kufunga wakuu wa giza(Anga)
na kuwaseta kuzimu
Marko.3:27, Mathayo 12:29.
Kabla sijaendelea labda
nikukumbushe kuwa hawa wakuu wa giza mara nyingi hukaa kwenye maeneo matatu
hapa duniani.
i).Kwenye Anga-roho hizi chafu
zinazotawala Eneo kubwa mfano; nchi, miji n.k hukaa kwenye Anga.
Mfano:Daniel 10:12-13,20.
-Mkuu wa ufalme wa uajemi
ii).Roho chafu zitawalazo ndani ya
kanisa familia n.k
-Hawa hukaa
ndani ya mtu kutokana na uhalali
walioupata kutoka kwa wazazi,mababu,na dhambi alizozitenda mtu huyo au
hukaa katika anga pia.
iii).Ardhini.
-uhalali wa
kukaa kwenye ardhi wanaupata kutokana na
matambiko,mazindiko
na makafara yanayotolewa kila siku.
Mfano: marko.5 yule mtu aliyemilikiwa na jeshi
la mapepo.
UFANYE NINI ILI UFANIKISHE
UTEKAJI WA MJI HUO.
Sasa basi ili uweze kuteka
mji,anga n.k na kuumiliki ni lazima kwanza uwe umeshafanya toba ya Damu ya
Yesu, kwa ajili -yako,ndugu zako na kuachilia ulinzi wa Damu ya Yesu}
mji,anga,ardhi na kwa ajili ya watu wa mji huo.Hatua ya pili ni kuvaa silaha[Efeso.6:13-18]Baada ya hayo sasa
umfunge mtu mwenye nguvu-mkuu
wa giza(Anga) wa eneo hilo-[Mathayo.
12:29] kwa kutumia funguo (mamlaka) uliyopewa na Yesu;ya kufunga na kufungua[Mathayo. 16:19].
-Na ndio maana Yesu
alitufundisha mbinu za kufanya ili tuweze kuteka eneo lolote,kupitia kitabu cha
marko.3:27,mathayo 12:29.
“Hawezi
mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu,na kuviteka vitu
vyake,asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu;ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
-Pia Yesu alitupa nguvu ya kufunga na
kufungua jambo lolote la adui.
Mathayo 16:18-19 “Nami
nitakupa wewe funguo za ufalme mbinguni;na lolote utakalolifunga
duniani,litakuwa limefungwa mbinguni;na lolote utakalolifungua duniani,litakuwa
limefunguliwa mbinguni”.
Pia anasema milango ya
kuzimu haitalishinda kanisa langu.
-Na tayari Bwana
alishasema kuwa atatupa sisi tulio wa uzao wa Ibrahimu kumiliki malango ya Adui
zetu.
Mwanzo
22:17. “…….na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”
v Mungu ametuokoa ili tuanze kueneza ufalme wake; na ili
kueneza ufalme wa Mungu ni lazima tuteke miji na maeneo mbali mbali ili yaweze
kuwa chini ya ufalme wa Mungu.Kwa hiyo kila eneo unalokwenda ni lazima uliteke
na kulimiliki kwa ajili ya ufalme wa MUNGU.
v Tumezaliwa tuwe washindi na watekaji wa
mji(conquerors)[Rumi.8:37,Mwanzo 24:60,1Yoh. 5:4]
v Kila mahali unapokanyaga, Bwana amekupa wewe kumiliki.Joshua
1:3
v Pia Yesu ametupa sisi mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka na
nguvu zote za yule Adui na hakuna kitakachotuzuru
Luka .10:19; Rumi. 16:20
-Miji tunayoishi ni lazima ifikie hatua iitwe kwa jina la Bwana
.Eze.45:35- na sio kwa jina la mapepo kama ilivyokuwa kwa Babeli[Ufunuo.18:2] “…umeanguka,umeanguka Babeli ule mkuu;umekuwa maskani ya mashetani,na
ngome ya kila roho mchafu,na kila ndege mchafu mwenye kuchukiza”
-Mji unapokosa maombi
unakuwa ni ngome ya mapepo kama ilivyo kuwa kwa babel.
NB:Mji unapokosa maombi unakuwa kama jalala la kila aina uchafu wa
dhambi.Unajua,mapepo ninayafananisha na nzi au panya-kwa kawaida huwezi ukakuta
nzi,panya mahali palipo pasafi mara nyingi utawakuta sehemu chafuchafu kama
jalalani.Wanachofuata inzi ni uchafu na ndivyo walivyo mapepo na majini.Mahali
ambapo maombi ya toba ya Damu ya Yesu yanafanyika kila siku,sio rahisi ukute
utawala wa shetani.
KANUNI YA
MAOMBI HAYA NI:-
·
Mathayo
12:29 + Mathayo 16:18-19=mathayo.6:9b-10
KUFUNGA (BINDING).
Tunapozungumzia suala la kufunga, hapa maana yake ni kama vile
unavyomkamata mwizi alafu ukamfunga miguu na mikono –ndivyo unavyotakiwa
kuwafunga hawa watu wenye nguvu
(roho zitawalazo) mathayo. 12:29.
Tunajua kuwa Yesu
alikuja ili kuzivunja kazi za adui-ibilisi. 1Yohana 3:8
Kufungua
(loosing).
Shetani huwa anatabia ya
kufunga watu kwa roho za mauti,magonjwa, uzinzi n.k.Kwa hiyo umepewa fursa hizo
ili uwafungue watu waliofungwa-isaya.61:1-4.
-Neno la Mungu ni
silaha,upanga wa roho.
·
Luka
13:11-12, 15-16
·
Efeso.6:17b,
ebra.4:12
·
-Fahamu jambo hili kwenye vita hii unachokiri/kisema kwa
kinywa chako kinakwenda kuwa cha kwako-ukikiri kushindwa lazima utashindwa tu.ufunuo.12:11
″ nao wakamshinda kwa damu ya
mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao″
Kwa hiyo =NENO + DAMUYA YESU=USHINDI.
Mathayo 4:1-11.
Yesu alimshinda shetani kwa
kutumia upanga wa roho (Neno la Mungu).Kwa hiyo hakikisha kuwa umejaa neno
ndani yako na ulitumie neno kwenye maombi yako ya kufunga hao watu wenye nguvu. mathayo. 12:29.
HUU NI MFANO MZURI WA MAOMBI YA
KUMFUNGA MTU MWENYE
NGUVU(mfano.Belizebul-kumfunga belzebuli)
-Kumbuka kabla ya maombi
haya hakikisha umeshafanya toba kama ya Daniel.9 alafu sasa ujivike silaha za
Mungu-Efeso.6:13-18. tamka
kwa kinywa chako mwenyewe kuwa “ninajifunga
mshipi wa kweli kiunoni mwangu kwa jina la Yesu,navaa drii ya haki kifuani
mwangu,najifungia utayari miguuni mwangu kwa ajili ya injili ya amani,zaidi ya
yote ninatwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo nitaizima mishale yote yenye moto
ya yule mwovu,napokea chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni neno la
Mungu,nami nadumu katika sala zote na maombi nikisali kila wakati katika Roho…”
-Baada ya hapo anza kufunga mkuu wa
Anga na baada ya hapo fanya unachotaka kama ni kubomoa-bomoa, kuharibu-haribu
na kisha,angamiza n.k.lakini usisahau
kujenga na kupanda kitu,kila unapobomoa na kuharibu na kuangamiza.
Mfano.umevunja roho ya mauti –hakikisha
unatamka(unapanda)roho ya uzima.[Yer.1:10,12,Yoh.10:10b]
Huu ni mfano wa maombi haya;
Omba hivi:-
Ninafunga roho ya uchawi iliyokaa
katika Anga kwa minyororo na kwa pingu za chuma zitokazo mbinguni .Ninasimama
katika neno la Mungu la Math.16:18-19.ambao unasema “ nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa Mbinguni na
kila utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni- (Math.16:19) nami ninakufunga mikono na miguu kwa jina
la Yesu na kwa hilo neno la BWANA.Nami ninakata kila kiunganishi chochote
kinachounganisha mkuu wa mapepo( rulling spirit-mkuu wao)na mapepo madogomadogo
.Nami ninakung’oa wewe mkuu wa giza katika
anga hili ninakushusha na kukukanyaga katika jina la Yesu.Ninalitakasa Anga
hili kwa Damu ya Yesu, nami namkabidhi Roho mtakatifu achukue nafasi ya kuwa
mkuu wa Anga la Eneo(taja jina la eneo unaloliombea)
- Nami ninavunja
roho za zote za ajali, mauti, uchawi, mafarakano, uzinzi, matambiko na makafara
kwa damu ya Yesu ninateketeza na
kuziharibu kwa jina la Yesu kristo.maana mimi ni rungu la bwana sawasawa naYeremia 51:20-23 Bwana
ameniweka ili kuvunja vunja kazi zako,kama neno lake linavosema katika -1Yohana 3:8 “kwamba
kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili apate kuzivunja kazi zote za
ibilisi shetani “nami kwa Damu Yesu ninavunja kazi zako zote juu ya maisha
yangu,mji huu,biashara yangu,afya yangu n.k.
-Nami katika jina la
Yesu ninajifunika na kujificha ndani ya damu ya YESU,Ee Mungu ninaomba
unizungushie ukuta wa moto sawaswa na neno lako la zekaria.2:5.Ninampinga
shetani na roho zake zote za malipizi na visasi alizozikusuda juu yangu na juu
ya ndugu zangu,biashara yangu,masomo yangu,afya yangu na chochote kilicho chini
yangu;shetani ninakutangazia kuwa huna mamlaka juu yake kwa jina na kwa Damu ya
YESU.Ninasimamia neno la bwana la Isaya.54:14-17
linalosema(soma)katika jina la Yesu nimeomba na kushukuru ameni”
Nb:Huu ni msingi tu wa kukusaidia
kuanzia; ila haufungwi kutumia kanuni nyingine
ambazo Roho mtakatifu atakufundisha kupitia kusoma kwako neno.
MUHIMU:Baada ya Maombi
hayo:-
·
Omba ulinzi wa Mungu juu yako na juu ya ndugu zako.
·
Vunja roho zote za malipizi na visasi vinavyokusudiwa na
Adui juu ya maisha yako na ndugu zako
·
Soma neno hili-
Isaya 54:14-17(ulinzi dhidi ya roho za malipizi na visasi)[Zekaria 2:5]
-Mshukuru Mungu kwa kuwa ameshajibu
maombi yako katika jina la Yesu.
SHORT SUMMARY.
MFUMO WA MAOMBI
YAKO(MTIRIRIKO) UNATAKIWA UWE HIVI:-
A.Toba ya Damu
ya Yesu
–Isa.1:18,43:25
·
Tubu kwa ajili ya ndugu zako,wewe mwenyewe marafiki na
watu wote wa karibu yako,omba ulinzi
kwa ajili yako na ndugu zako.
·
Tubu kwa ajili ya Mji wako,Anga lake ,Ardhi n.k. takasa na umwage Damu ya Yesu ya ulinzi ya
kufunika Anga,Mji,Ardhi,Barabara,maji n.k
B.KUOMBEA MJI,KANISA FAMILIA N.K
-Tumia funguo za Mathayo 16:19,18:18 funga wakuu wa giza
,Anga na mapepo wabaya kwenye Anga n.k
Wasete kuzimu kwa jina na kwa Damu
ya YESU.
-kata kila connection(kiunganishi)
inayowaunganisha wakuu wa giza na mapepo wadogowadogo.
-vunja kazi za ibilisi [1Yohana3:8,Yeremia 51:20-23]
C.HITIMISHO.
Ulinzi juu yako, ndugu zako ,vunja
roho ya malipizi na visasi-Isa.54:14
17. “……watu watakaokusanyana juu yako wataanguka……….kila silaha
itakayofanyika juu yako haitafanikiwa…..”
Nb:Kama bado maneno hayo yote ya
biblia hayajakaa kichwani,basi hakikisha unakuwa na biblia karibu; kila
unapofanya maombi yako ya aina hii.
Neno
la Mwisho.
Maombi yako ni ya muhimu
sana kwa ajili ya huduma hii kuendelea kusonga mbele.philip.3:13-14. “Ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba
nimekwisha kushika ila natenda neno moja tu;…nikiyachuchumilia yaliyo
mbele;nakaza mwendo nifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika
kristo Yesu”
Kwa maoni na ushauri na maswali ;
JESUS ACTS MINISTRIES &JESUS
BLOOD’S
INTERCESSORY MINISTRIES.[JAM &JBIM]
Mwl.loyshiye.k.mollel
Mob.+255762568280
