Thursday, April 12, 2012

MAOMBI YA KUMILIKI MJI



                  UMUHIMU WA KUUOMBEA ENEO/MJI UNAOISHI  KWA AJILI YA KUUMILIKI
                   [KANUNI ZA KUTEKA MIJI KWA AJILI YA BWANA, KWA NJIA YA
                     MAOMBI.TOLEO LA PILI 2012 ]                                                                                     
                                                  UTANGULIZI
                               Ndugu mpendwa napenda kukusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Pia ninapenda kukukaribisha katika kujifunza somo hili.Somo hili lina umuhimu mkubwa sana katika nyakati/majira       tuliyopo sasa.Kama kichwa cha somo kinavyoonyesha,somo hili ni somo ambalo naamini litakwenda kuleta mapinduzi ya kiroho katika jamii,familia na kanisa kwa ujumla.Nakushauri ulisome somo hili kwa mtiririko ili uweze kupata maarifa mapya na vitu vipya kutoka kwa Roho Mtakatifu.Lengo la kwanza la somo hili ni kukuandaa kama mwanajeshi wa Bwana,kwa ajili ya kuteka miji iliyo chini ya shetani na kuirejeza kwenye ufalme wa Mungu Baba.Sasa unaweza ukawa unajiuliza,swali hili;kwamba kwa nini mimi ndio niteke miji hiyo?kwanini Mungu mwenyewe asifanye kazi hiyo?Jibu ni kwamba Mungu huwa anafanya kazi pamoja nasi kwa ajili ya kutupatia mema[Rumi.8:28],Na mema hayawezi kuja kama miji tunayoishi itaendelea kuwa chini ya ufalme wa giza.Kwa nini tuteke miji wakati,aliyeumba miji yote ni Mungu  na wala sio shetani?  
                               Dhambi ya Adamu na Eva pale eden ilipelekea dunia yote kuwa chini ya shetani(yaani shetani akawa ndio mungu wa dunia hii)[2kor.4:4] badala ya mwanadamu. Kwa hiyo asilimia kubwa ya miji tunayoishi inamilikiwa na adui(shetani).Na ndio maana kazi ya Mungu inapigwa vita kwa kiasi kikubwa.Sasa lengo la pili la somo hili ni kukuwekea(impart knowledge) ufahamu utakaokusaidia kuirejeza miji hiyo mikononi mwako,kama mwakilishi wa ufalme wa Mungu.Kutokana na miji mingi kuwa chini ya shetani,matukio mengi ya kutisha yamekuwa yakitokea kila siku,mfano vifo vya ajabu,ajali za barabarani,mauaji ya albino nk.
                            Sasa shetani amekuwa akipofusha watu ili watu wasijue kuwa yeye(shetani) ndiye anayehusika katika matukio hayo yasiyo na hata chembe ya huruma[Mungu ni mwenye huruma] hawezi amuru maalbino wauae,ajali za watu kufa kama vile kuku kwa mkupuo.Ndugu mpendwa shetani ni mjanja na biblia inasema kwenye kitabu cha ufunuo kuwa anajua wakati uliobaki ni mchache..kwa hiyo anachofanya ni kuhakikisha anav
                  Ni muda mrefu sana nimekuwa nikisikia matukio mengi ya kutisha na ya  ajabu yakitokea katika jamii tunazoishi; hasahasa matukio ya ajali za barabarani, ukatili , watu kujinyonga na kunywa sumu nk.Na mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wengi wakisema yote hayo ni mapenzi ya Mungu(yaani Mungu ndio amesababisha) na muda mwingine hata watumishi wa Mungu wengi wakati wa mazishi nimewasikia na wewe umewasikia wakisema “Bwana ametoa na Bwana ametwaa;jina la Bwana libarikiwe”
                             Kwa upande wangu nimekuwa nikipata shida kidogo juu ya misemo hii  ya mazishi, na Je ni kweli Bwana ndiye anayetwaa hao watu wote? mfano mlevi,ajali nk.Maana muda mwingine unakuta wala Mungu hahusiki hata kidogo katika matukio hayo, bali aiza mtu amejisababishia mwenyewe au kuna mkono wa shetani umehusika!.Si kwamba nasema Mungu hahusiki kwa asilimia zote,hapana!.Bali ukikuta Mungu amehusika basi mtu huyo amekuwa mgumu sana na amekuwa akiharibu kazi ya Mungu mfano,Herode[Matendo.12:22-23] au Mungu amependa kumpumzisha mtu huyo kwasababu ya umri[1Fal.1:1,1nyak.29:28 .
                            Kumbuka kuwa si mapenzi ya Mungu mtu afe katika       dhambi[Eze.18:23; 33:11], pia si mapenzi ya Mungu ufe kabla ya wakati ambao yeye amekusudia uishi hapa duniani ambao ni miaka 120[Mwanzo.6:3] kama ukiishi vizuri na Bwana hiki ni kiwango cha chini tu unaweza ukaishi zaidi ya hapo mfano ibrahimu aliishi miaka 140,Ayubu 140.Sasa kama ndio hivyo kwa nini uondoke kabla ya hapo.
                             Sio hivyo tu bali kwa wewe mtumishi wa Mungu uwepo wako hapa duniani ni wa muhimu sana,Yesu alimwomba Baba wa mbinguni ili asitutoe ulimwenguni [Yoh.17:15] , maana yake kuna kazi unatakiwa ufanye,na endapo utaonekana huifanyi na wala humzalii Mungu matunda basi ndio unakatwa[Math.3:11,7:19; Luka.13:6-9](sasa hii ni kwa ajili ya wale tu ya waliokoka).ni kweli kufa ni faida kwa mtu aliyeokoka,hilo nakubaliana nalo asilimia zote,lakini pia kuishi ni kristo na kwafaa sana kubaki kwa ajili ya kristo na ili kuendelea kuziremba taji zetu za kule mbinguni(kumbuka kuwa utalipwa kwa ajili ya kazi unayofanya hapa Duniani,utavalishwa taji,kama ukienda huko na hakuna matunda yoyote uliyomzalia Mungu basi usitarajie kitu.
                               Unajua utakuwaje?Embu fikiria unahitimu kidato cha 4/6 au chuo alafu siku hiyo wenzako wote wanapewa zawadi na kuvalishwa taji, alafu wewe peke yako tu ,ndio huna mtu wa kukuvalisha taji wala kukupa zawadi,unafikiri utajisikiaje?lazima ujisikie vibaya.Ndivyo itakavyokuwa unavyong’ang’ania kufa ukisema ni faida wakati hamna chochote ulichokifanya hapa duniani kwa ajili ya Mungu[Luka.12:47-48].
                                Ujue hii inakuhusu wewe ndugu uliyeokoka na lengo langu hapa ni kuona unabadilisha mawazo uliyonayo na maombi ambayo umekuwa ukimwomba Mungu ili akuondoe duniani.Kumbuka kuwa Mungu anakuhitaji ili uendelee kuwepo hapa duniani kwa aijli ya kazi yake[Yoh.17:15].Wewe ukifa shetani anafurahia kwa sababu upinzani unapungua.Hivyo badilisha hayo mawazo ya kutaka kuondoka(kufa) bali umwombe Mungu akuongezee siku za kuishi angalau na wewe ujitengenezee taji yako kule mbinguni[Ufunuo.2,3].
                            Sasa kwa watu ambao hawajaokoka Mungu anasema anachukia kufa kwao katika dhambi,na kwasababu hiyo basi inamanisha kuwa Mungu hahusiki katika vifo vingi vya watu wanaokufa kabla ya wakati uliokusudiwa.Na ukijaribu kuchunguza kwa undani zaidi utakuta asilmia kubwa ya ajali na vifo vinavyotokea nyakati za leo, wala Mungu hahusiki na kama anahusika naweza nikasema kuwa ni kwa asilimia chache sana( 25%) tu tena hiki ni kiwango kikubwa sana.Embu fikiria  vifo vya maalibino,watoto wachanga,vijana wadogo,Ajali za kila siku barabarani na watu kujinyonga na kunywa sumu je haya yote utasema Mungu anahusika?
                            Sasa usishtuke maana lengo la somo hili sio kukuogopesha bali somo hili lengo lake kubwa ni kufuta mawazo hasi(potofu) uliyojengewa na watu kuhusu masuala hayo na upate ufahamu mpya(chanya) ili uweze kuchukua hatua ambazo Mungu anataka wewe uzichukue ili angalau wewe uweze fikisha siku za Bwana.
                             NB:Kuna watu ambao mmekuwa na mawazo potofu,eti kwamba ukifundisha mafundisho kama haya una mtukuza shetani sana kwasababu yeye ndiye anatajwa mara nyingi.Nani kakudanganya kuwa unapomtaja mtu kwa ubaya,kwa lengo la kufichua maovu yake,ni kwamba unamsifia?.Siri ya vita vyote sikuzote ni kumsoma adui yako na kumsoma adui yako haimaanishi unamtukuza.Ndugu kama na wew ulikuwa na mawazo kama haya uyaondoe,maana hayatoki kwa Mungu bali kwa shetani ; kwa lengo la kukufanya usizijue hila zake na ili aendelee kukutawala na kutawala mji unaoishi.
                             Kanuni ya kusoma somo hili ni kwamba kabla haujaendelea na somo hili nakusihi ufanye maombi kwanza umuombe Roho mtakatifu akupe kiu ya kujifunza somo hili na nguvu ya kulitendea kazi [soma Mt.7:24-27; 13:18-23] maana somo hili lina upinzani sana.mpaka nimeweza kuliandaa somo hili ni kwa neema ya Mungu tu na kama sio neema hiyo basi sasa hivi usingekuwa na nakala hii.Hivyo anza kwa maombi,haribu na uvunje kila roho zilizotumwa na mwovu ili kukuzuia usipate kitu katika somo hili.Pia uwe na biblia yako karibu.Somo hili limegawanyika katika sehemu kuu tano (5); sehemu ya kwanza ,ya pili ,ya tatu,nne,tano na hitimisho.

                                 SEHEMU YA KWANZA:KUJITAMBUA NA KUTAMBUA
                               Somo hili limekuja wakati muafaka ambao wewe kama mtu wa Mungu unatakiwa ujitambue wewe ni nani,unapambana nanani(adui)? ;na ni nini unatakiwa kufanya katika nyakati hizi za mwisho.
                             Tunaposema kujitambua inamaanisha kuwa wewe mtu wa Mungu unatakiwa kujitambua kuwa wewe ni nani mbele za Mungu na nini unatakiwa kufanya.Na tunaposema kutambua maana yake unapaswa kujua adui yako ni nani?,na ni majira gani uliyoko?
                             Na nianze kwa kusema kwamba shida kubwa iliyoko katikati ya wana wa Mungu(waliookoka) ni kutokujua majira waliyoko na hata kama wanajua wanashindwa kutambua ninini wanachotakiwa kufanya kwenye majira hayo[Efeso.5:15-21].Wapendwa wengi nyakati za leo wamejikita zaidi kwenye kuombea masuala ya kwao na ya madhehebu ya kwao.Wamesahau kuwa nini Yesu aliwaagiza(The great commission) [Mathayo.24:14]..Kumbuka kuwa Yesu alisema kwamba ; “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..”[Mathayo.28:19-20].
                             Lakini wapendwa wengi swala hili hawana mpango nalo ,badala yake wamegeuka na kuwa kama wanasiasa ambao badala ya kuwatetea  wananchi waliowachagua,wananza kutetea vyama vyao;na ndivyo walivyo watumishi na wapendwa wengi wa leo.badala ya kumtetea Yesu aliyewatuma wanaanza kutetea madhehebu ya yao.Hii yote ni kutokujitambua na kutokutambua mapenzi ya Bwana wao[Luka.12:47-48].
                               Biblia inasema katika kitabu cha [Ufunuo.12:12b].“Ole wa nchi    na bahari! kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi ,akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”Biblia inaweka wazi kuwa shetani yeye anajua majira aliyoko na anayatumia vizuri…Kanisa la leo limesahau na hata kama halijasahau basi limeacha wajibu wake na kazi ambayo Mungu alikusudia kanisa lifanye(The great commission)[Mathayo.24:14].
                             Kila kanisa(madhehebu) leo hii, limejiwekea vipao mbele vyake katika mambo yao.Lakini masuala ya Mungu wameyaweka pembeni.Kanisa la leo halina muda wa kutafuta mapenzi ya Mungu.Ukikuta mipango wanayopanga ni ya kwao binafsi na hata ukikuta mahubiri wanayoyafundisha ni ya kusengenya kanisa lingine,wakifikiri kuwa wanapatia kumbe wanakosea w.Kanisa la mitume halikuwa na tabia hizi za leo.
                              Na kwa sababu hiyo tunahitaji matenge wanasahau kuwa Yesu alisema; “……na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..”[Mathayo.28:19-20] ikiwemo upedo[Yoh.13:34-35],kupenda jirani na Adui yako[Matthayo.5:43-48].Kanisa la leo linahitaji matengenezo(reformation) mapya kama yale aliyoyafanya mtumishi wa Mungu Martin Luther.Kanisa la leo halina umoja,halina upendo, halina unyenyekevu ,wala uvumilivu na kusamehana nk.Zaidi sana ubinafsi na kusengenyana ndio kumejaa makanisani Kwakweli kanisa linapaswa kutubu na kurudi kwenye kusudi ambalo Mungu alikusudia kanisa lifanye.
                               Sasa unaweza ukaanza kufikiria kuwa ninalalama bure hapana! Ila nakufundisha kitu ambacho kipo kwenye biblia.Wala  sio nimebuni.sasa tufuatane nikupitishe kwenye maandiko ili upate kujua nini ,Mungu alikusudia kwa ajili ya kanisa;alafu linganisha na jinsi kanisa la leo linavyoishi.Sasa tuanzie mwanzo kabisa wa nini ambacho Mungu alikuwa anakusudia kwa ajili ya kanisa:-
                               Kitabu cha [mwanzo.1:26-28] kinaonyesha mwanzo wa uumbaji wa Mungu wa kumuumba mwanadamu.Mungu anasema ″Na tufanye mtu kwa mfano wetu ;na kwa sura yetu ;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani ;na wanyama ;na nchi yote pia;na kila chenye   kutambaa kitambaacho juu ya nchi……″

                       Lengo  kubwa la Mungu kuumba Dunia ni kwa ajili ya mwanadamu na ndio maana aliweka kila kitu cha kumsaidia na cha kumfaa mwanadamu katika maisha yake ;kabla hajaumbwa aliwekewa hewa –oksjeni;maji;miti;mifugo;mimea n.k.Vyote hivi ni kwa ajili ya mwanadamu.
                               Na baada ya Bwana Mungu kumuumba mwanadamu alimkabidhi utawala na umiliki wa Dunia hii.Alipewa kumiliki dunia na vyote vilivyomo ndani yake- [Mwanzo1: 27-28].“Mungu akawabarikia……na kuitiisha ;mkatawale……na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi ″.Neno ninalotaka ulione hapo kwenye mistari hiyo ni “kutiisha na kutawala dunia”
                             Wakati huohuo ndani ya Dunia pia alikuwemo shetan, kwa sababu tayari alishahasi kule mbinguni na akatupwa Duniani.soma-[Isaya.14:12-15,Eze.28:11-19].        
                       [Ufunuo. 12:10.]“………kwa maana ametupwa chini mshitaki      wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wet,u mchana na usiku ″.
                             Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa nafasi moja ya heshima na kubwa sana –na nafasi hiyo ni ya umiliki wa Dunia hii-Na kwa ujumla hakuna malaika yeyote aliyewahi kupewa nafasi kama aliyopewa mwanadamu,hata shetani enzi za uhai wake (kule mbinguni) hakuwahi kupata nafasi kama hiyo, japo aliitamani sana na ndio maana alifanya uhasi akifikiri kuwa angepata sehemu ya kumiliki, na yeye awe kama Mungu.
                              Katika ranking(ngazi) ya ufalme wa Mungu hapa duniani, mwanadamu alipewa nafasi ya pili-yaani baada ya Mungu alifuata mwanadamu;alafu malaika na mwisho ni shetani na mapepo yake .      Tazama mchoro huu hapo chini:-

MUNGU
BABA+MWANA +ROHO MTAKATIFU
                                                ↓                
MWANADAMU
MME  +  MKE
                                                 ↓
MALAIKA
             
Shetani


           A: Mwanadamu.
          i)Zab.8:4-6:
          ″…….umemfanya mdogo punde kuliko  Mungu…umevitia vitu vyote chini ya miguu yake………Ndege wa angani………..na kila kipitacho  njia za baharini. ″
           ii)Ebrania 2:7
                              ″………″umemfanya mdogo punde kuliko malaika umemvika taji ya utukufu na heshima………″
                  -Maandiko yote hapo juu yanaonyesha jinsi mchoro unavyoelezea pale  juu.
                             Yaani japo mwanadamu ameonekana ni mdogo;lakini mbele za Mungu yeye ana nafasi ya juu sana katika dunia hii.Mchoro huu ni baada ya Mungu  kuumba dunia na kumweka mwanadamu ndani ya dunia.
                              Mwanzo .3 -Inatuonyesha kilichotokea ndani ya Bustani ya edeni–kama nilivyokuambia kuwa shetani tayari alishakuwepo ndani ya dunia –na wala hakufurahia hata kidogo nafasi aliyopewa mwanadamu – na vile vile hakuwa tayari  kuwa chini(kutawaliwa)ya mwanadamu .
                            Kumbuka kuwa wakati Mungu anampa Adam maagizo ya kutokula matunda ya mti wakatikati wa ujuzi wa mema na mabaya, Hawa/Eva alikuwa bado hajaumbwa-[Mwanzo.2:16-17,18-25].Kwa hiyo wakati Mungu anatoa hayo maagizo shetani alikuwa anasikia maana alikuwepo.Na yeye(shetani) alikuwa anajua kuwa Eva hakuwepo wakati Mungu akitoa maagizo hayo,ila Eva alipata kujua hayo kutoka kwa Adam,Kwa hiyo alitumia nafasi hiyo kutunga hila ya kumdanganya nayo mwanadamu ili yeye aipate hiyo nafasi ya utawala wa Dunia hii.
                            Shetani alijua fika kuwa Mungu aliwaambia wasile matunda ya mti wa mema na mabaya; ila alitumia maneno haya ya hila“ati hivi ndivyo alivyosema Mungu msile matunda ya miti yote bustanini? …hakika hamtakufa…mtakuwa kama Mungu” kwa lengo la kuwadanganya na kuwaingiza katika dhambi ya uhasi ambayo na yeye aliifanya kule mbinguni akatupwa chini-[Isaya.14:13-14].               
                            Mwanzo 3:1-4.Kitendo cha Eva kuyaamini maneno ya shetani ni kwasababu alisikia kuwa akila hayo matunda na yeye atakuwa kama Mungu,kwa hiyo na yeye alikuwa anataka awe kama Mungu,kama vilevile shetani naye alivyotaka kumpindua Mungu ili yeye ndiye awe Mungu m kuu,matokeo yake akatupwa chini.
                            Sasa matokeo ya dhambi waliyofanya Adam na Hawa kulibadilisha muonekano wa ule mchoro wa pale juu wa utawala wa Dunia hii  - Dhambi ile, ilimpa shetani nafasi ya kumiliki na kutawala Dunia hii badala ya mwanadamu. Hata ule mchoro nao ukabadilika. Na ukawa kama hivi:-

                         MUNGU
BABA + MWANA+ ROHO MTAKATIFU                       
                                                    
SHETANI

MALAIKA
MWANADAMU
MME  +  MKE

                            Na kwasababu hiyo basi; dhambi hiyo ikasababisha mwanadamu kuwa chini ya shetani na malaika pia –na ndio maana, [Yuda 1:9] 
                     ″…….lakini mikaeli malaika mkuu…hakuthubutu kumshitaki (shetani)……Bali alisema Bwana na akukemee″.
                            Maneno haya ya malaika mikaeli yanaonyesha dhahiri effect(matokeo) ya dhambi iliyotokea bustanini kiasi kwamba malaika hawakuwa na uwezo wa kumkemea shetani – kwa nini?_____Jibu ni kwa sababu shetani ndiye amechukua ile nafasi ya mwanadamu kama mchoro unavyoonyesha hapo juu.
                             Kwa hiyo baada ya mwanadamu kupoteza nafasi aliyopewa na Mungu ya kutawala dunia hii,ilimlazimu Mungu atafute njia ya kumsaidia mwanadanu ili aweze kurudi kwenye nafasi yake ya mwanzoni.Maana alishapoteza baada ya kutenda dhambi na ndio maana Mungu alipomtembelea bustanini aliita akisema Adam,Adam uko wapi? Maana yake Mungu alikuta kitu kingine(shetani) kwenye nafasi ya Adam.
                            Hivyo Mungu akaanza kuweka mipango ya kumkomboa mwanadamu kutoka mikononi mwa shetani na amrudishe kwenye postion(nafasi) yake ya mwanzo.Mpango kwa lugha ya kingereza unaitwa “plan” ukisoma kamusi ya kingereza ya Oxford toleo la 7 inaelezea vizuri maana ya plan(mpango).Na katika kupanga mipango ili kufikia kusudio fulani, huwa ni lazima uwe na plan A na plan B.Hii inamaanisha kuwa plan A ikifeli(shindwa) plan B inaingizwa kazini.Sasa plan B kwa jina lingine inajulikana kama “MASTER PLAN” na mfano mzuri wa plan B ni sawasawa na kazi ya gear(gia) namba moja ya kwenye gari na kwa kawaida sikuzote inapofika kwenye mwinuko mkali,gia zingine zitashindwa lakini namba moja yenyewe haitashindwa labda hilo gari liwe ni bovu.
           Sasa usije ukafikiri kuwa nafundisha maswala udereva  wa magari! Hapana!.Ninachotaka hapa ni ili uelewe vizuri plan(mpango)A wa Mungu na plan B(Master plan) ya Mungu katika kumrudishia mwanadamu utawala wa dunia hii.
                   Sasa embu tuangalie plan zote mbili jinsi zilivyofanya kazi:-

                   PLAN A:MPANGO “A” WA MUNGU KUMRUDISHIA
                          MWANADAMU UTAWALA WA DUNIA HII.                 
             Baada ya Mungu kuona kuwa Mwanadam ameshapoteza nafasi aliyokuwa amempa,ikabidi Mungu aingize plan A kazini,na mpango huu aliuanzia kwa Ibraham-Isaka-Yakobo→Musa→Daudi.Kipindi cha Musa Mungu alimwagiza Musa ajenge hema na aweke makuhani na damu ya makondoo na mafahali ilitumika katika kuwapatanisha wanadamu na Mungu na kuwafanya wapate nafasi ya kutawala tena-(Kutoka.25,27,27,28).
                                 Lakini pamoja na hayo yote mpango huu(plan A) haukuweza kufanikisha lile kusudi la Mungu la kumrudishia mwanadamu nafasi aliyoipoteza,damu za wanyama hazikuweza kumbadilisha mtu kutoka kwenye dhambi alizokuwa nazo mfano:mtu mlevi au mzinzi kuachana na tabia hizo alizonazo,Sio hivyo tu bali damu hizo za makondoo na mafahali hazikuwa na uwezo wa kumshinda shetani; shetani aliendelea kujitapa na kujiita yeye ndiye mungu wa dunia hii.Hata yale matokeo mabaya yaliyosababishwa na dhambi ya bustanini,hii kama vile magonjwa(ukoma)- plan A, ya damu za mafahali na makondoo haikuweza kuondoa magonjwa hayo, watu waliendelea kuteseka na magonjwa yao bila msaada wowote na ikafikia hatua hata yaw engine kutengwa na jamii ili wasiwaambukize wengine.[2falme.7:3].
                                 Kwa hiyo kila mtu alipokuwa akitenda dhambi ilimbidi atafute kondoo wa kumpeleka kwa kuhani ili akasamehewe dhambi zake[Lawi.5:1-10].Kwa hiyo kila siku damu za makondoo na mafahali zilikuwa zikimwagika hekaluni; lakini hata hivyo plan “A” haikufanikiwa.Na katika plan hii Mungu aliwatuma manabii mbalimbali wengine waliuawa na kuteswa na Shetani akafikiri kuwa sasa yeye ameshindikana au amekuwa chronic.
                  Hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kukemea pepo kwasababu   damu hizi za wanyama hazikuwa na uwezo huo.

                                            SEHEMU YA PILI
                  PLAN B(MASTER   PLAN) -UJIO WA YESU NA MATOKEO YA KIFO CHAKE.                                   
                             Baada ya plan A kufeli Mungu akaamua aingize plan B kazini,Plan B hiyo ni Yesu-na mwili wake(kanisa) ambalo yeye mwenyewe amesema kwamba malango ya kuzimu hayatalishinda kanisa la Mungu.Na kama nilivyokuambia Hapo mwanzo kuwa plan B ndio “master plan” na kwa kawaida sikuzote plan B (master plan) huwa yenyewe haishindwi; yaani yenyewe ndio solution ya kila kitu.Kwa hiyo alichokifanya Mungu ni kuamua kuja mwenyewe ulimwenguni kumshughulikia shetani na kumpokonya ule ufalme aliouiba;na kumrudishia binadamu utawala wa dunia hii.Na ndio maana Yesu akaamua kuuvua utukufu wake na kuvaa utu ili tu aweze kutukomboa.Kwa sababu asingeweza kutukomboa bila ya yeye kuvaa ubinadamu.Kwa sababu ukombozi wetu ulihitaji Damu yenye nguvu kuliko ile ya mafahali na makondoo iliyotolewa enzi za agano la kale ambayo haikuweza kumsaidia mwanadam kushinda dhambi na shetani[Ebra.9:22b] inasema “na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo(la dhambi)”
                 Pia kuja kwake(Yesu) kwa namna ya mwili ni ili awe kielelezo cha sisi kuiga na kuishi maisha aliyoyaishi hapa duniani.Na ndio maana alikuja kwa namna ya mwili ili aweze kutuhubiria, kwa hiyo alipita kijiji baada ya kijiji akihubiri.Embu fikiria kwamba; je angekuja kwa namna ya kiungu ingekuwaje[kut.20:18-19] “…..na watu walipoona hayo wakatetemeka wakasimama mbali,…Musa sema nasi wewe ,nasi tutasikia,bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa”
                                 Kwa hiyo Mungu akaamua kuuvaa mwili ili aje atukomboe [filp.2:5-11,ebra.2:17;4:15] Hivyo ujio wa Yesu ulikuwa na kusudi la kutukomboa na kuturudishia ufalme na nafasi nyingine ya upatanisho(ukuhani).Huduma ya upatanisho iko ndani ya huduma ya ukuhani-[kut.32:30;2kor.5:18-19].Sasa fuatana nami,nitakueleza kazi ya huduma hii ya upatanisho ndani ya ukuhani inavyotakiwa kufanya kazi nyakati hizi za leo-[Ufu.59-10] inasema kwamba tumenunuliwa kwa damu ya Yesu na tukafanywa kuwa makuhani na ufalme kwa ajili ya Mungu wetu.[1petro.2:5,9-10].Kwa hiyo alichofanya Yesu ni kumwaga damu yake ambayo kwa hiyo damu sisi tumenunuliwa na baada ya kutununua akaturudishia ule ufalme tuliopokonywa na ibilisi hapo mwanzo kwa njia ya dhambi; na ili shetani asije akautwaa tena huo ufalme,Yesu aliamua kutuongezea huduma ya ukuhani kwa lengo la kulinda nafasi ya ufalme isije ikapotea tena.
                                  Huduma ya ufalme na ukuhani ni nafasi ambazo zinakwenda kwa pamoja na wala huwezi kuzitenganisha.Hivyo bila ukuhani, ufalme wetu hauwezi kuthibitika.Yaani ni sawasawa na mfalme asiye na walinzi au nchi isiyo na jeshi;na kwa namna hiyo kamwe ufalme huo au nchi ya namna hiyo ni rahisi sana kuvamiwa na kutekwa na kumilikiwa na maadui.Kwa hiyo huduma hii ya ukuhani ni ya muhimu sana katika kuhakikisha kuwa ufalme wako haupotei na wala adui hapati nafasi juu ya eneo unalotawala.Kumbuka kuwa wewe mtu uliyeokoka;Mungu anakutazama wewe kama mfalme wa eneo uliloko,hivyo na wewe unatakiwa ujione hivyohivyo kama jinsi vile Mungu anavyokuona na sio vinginevyo. Sasa kabla hatujaenda kuangalia nini maana ya kuwa mfalme,naomba tuangalie kwanza aina mbili za falme,katika ulimwengu wa roho.
                                 Katika ulimwengu wa roho kuna ufalme wa nuru au wa Mungu na ufalme wa pili ni ufalme wa giza(shetani).Falme zote hizi mbili zinatafuta nafasi ya kuimiliki dunia hii.Na ili kuimiliki dunia hii ni lazima mwanadamu ahusishwe.Kwa hiyo ufalme wa Mungu unatafuta watu ambao watasimama kwa niaba ya ufalme wa Mungu ili waimiliki dunia-na mmoja wa watu hao ambao ufalme wa Mungu unawatafuta ni wewe mpendwa uliyeokoka.Sasa shetani naye anawatafuta watu watakaolisimamia kusudi lake,ili ufalme wake ufanikiwe…kipengele hiki cha falme mbili kitaedelea sehemu ya tatu(3).
                                 Kwa hiyo ujio wa Yesu ulileta mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu wa roho.Na kitu alichokifanya Yesu ni kumnyang’anya shetani ile nafasi  (ufalme/utawala) aliyoiiba kwa hila pale bustanini Edeni –[Mwanzo .3 ]na kumrudishia mwanadamu.kwa hiyo Yesu alimtoa shetani katika hiyo nafasi alafu akatuchukua na kuturudishia ile nafasi yetu ambayo Mungu alikusudia tuwe nayo tokea awali,yaani nafasi ya kumiliki dunia-[Mwanzo 1:28].
                                Ufunuo 5:9-10.inasema hivi:-
                   ″…………kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na Taifa (10)ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu;nao wanamiliki  juu ya nchi”.
                              Kitu alichokifanya Yesu ni kutukomboa kwa damu yake;alafu akaturudisha kwenye nafasi yetu ambayo Mungu alikusudia tuwe nayo tokea mwanzo wa uumbaji wake Mungu – yaani nafasi ya ufalme ya kumiliki na kutawala.[mwanzo.1:26-28].
                              
                                    KUWA MFALME MAANA YAKE NI NINI?
                          Kuwa mfalme maana yake wewe ndio mtawala wa eneo uliloko;iwe ni familia ,mji ,shule,kanisa,nchi nk.Na hii inamaanisha kuwa watu wote wa eneo hilo wako chini ya utawala wako,yaani ni raia wako; iwe ni ndugu zako au si ndugu zako.Sasa ni lazima ufahamu kuwa kila ufalme una mipaka yake na mipaka hiyo inaheshimiwa na kutambulika kisheria na kimataifa kuwa inamilikiwa na mfalme fulani.Na ili ufalme wako uwe  imara ni lazima:-
                         i)Uwe na mipaka yako inayotambuilika(miliki ardhi) kisheria.
                         ii)Uwe na watu  na pia watu hao uwe una uwezo wa kuwasaidia   kupata   mahitaji yao ya msingi.
                        iii)Miliki Anga+maji.
                                Hii inamaanisha kuwa lazima kuwe na ulinzi katika mipaka ya ardhi na pia juu ya mipaka ya anga lako.Kwa nini kuwe na ulinzi kwenye mipaka ya ufalme wako? Jibu lake ni hili-kwa nini Tanzania ina jeshi la ardhini,la maji na la anga?Sasa nakupa homework ya kujua kwa nini kuwe na jeshi la nchi kavu(ardhi),la maji na la anga katika Tanzania-ukipata jibu lake utatambua umuhimu wa kuwa na maombi ya kuombea anga,ardhi,maji na watu.Nchi ya Tanzania ina mipaka yake ya anga ambayo sio rahisi nchi nyingine iingilie bila ya idhini ya Tanzania.Na ndio maana sio rahisi uone ndege ya jeshi la Kenya ikiruka kwenye anga la Tanzania bila idhini ya Tanzania,ikitokea hivyo ujue huko niuchokozi wa vita.Sasa usifikiri kuwa nakufundisha siasa, hapana!, ila ninataka kupitia mifano hiyo ujue jinsi ulimwengu wa roho unavyofanya kazi.Hata Yesu alitumia mifano katika mafundisho yake.Hivyo wewe kama mfalme ni lazima utawale na kumiliki ardhi,watu wake na anga la sehemu unakoishi ili mambo yako na mipango yako iweze fanikiwa(yaani kuanzia sasa anza kujiona wewe ni mfalme wa Eneo uliloko; yaani familia yako/kanisa /mji/nchi nk. [Daniel.10:12-13;20]. 

                                KWA NINI WEWE NA SIO MALAIKA?
                          Huwa najiulizaga swali hili kwamba ni kwa nini Mungu ametuchagua sisi kuwa watawala wa dunia hii,kwa nini hajawachagua malaika kuchukua nafasi hii?.Kwa kweli  Mungu amekuheshimu sana akakupa nafasi hiyo kwa sababu  ya makusudi yake ,yaani Mungu alikusudia wewe uwe mungu wa dunia hii. Sasa ujio wa Yesu ulikuwa ni kuja kutimiza kile ambacho Mungu alikukusudia-Yohana.10:34-36.
 “Yesu akawajibu ,Je haikuandikwa katika korati yenu ya kwamba ,mimi nimesema ndinyi miungu?………….″ [source-Zab 82:6]
v Kwa hiyo yesu alipokuja alibadilisha mfumo wa utawala wa dunia  hii.ukawa kama uonekanavyo hapa chini.
                          MUNGU  
  BABA + MWANA+ ROHO MTAKATIFU                    
            ↓
    MWANADAMU
(ALIYEOKOKA)  
         ↓
MALAIKA
                                                      Inaendelea uk. Ujao…..
SHETANI
           ↓
WAOVU(watu)

                Kwa hiyo Yesu alituhamisha kutoka katika ufalme wa giza   (kutawaliwa na shetani)na kutuleta katika ufalme wa pendo lake.
                  [ Epheso 2:6]″……..akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa  roho katika kristo Yesu″.
                           
                              SASA ANZA KUJITAMBUA KUWA :-
Ø Wewe ni mfalme na kuhani wa Eneo unaloishi na wewe ndiwe     unayetakiwa umiliki hilo eneo.Ufu.5:9-10.kutoka19:6, 1petro 2:5,9-10.
Ø Wewe ni kiumbe kipya ndani ya kristo. 2korinto 5:17
Ø Wewe unazo funguo za ufalme wa mbinguni. mathayo 16:18-19;mathayo 18:18
                             Jambo lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa kule mbinguni .Kwa hiyo wewe  ndio mwenye maamuzi ya mwisho ya Eneo unaloishi.unaweza ukaamua shetani aendelee kutawala au asiendelee.
Ø wewe ni rungu na silaha za vita za Bwana –Jeremia 51:20-23.
                          -kazi yako kama rungu ni kuvunjavunja kazi za ibilisi-hiyo ndiyo kazi aliyokupa Yesu . Yohana.17:15,
                 -wewe upo hai na umeokoka kwa sababu ya makusudi fulani ndio maana yesu ameomba kwamba tusiondoke katika ulimwengu huu.
                         1Yohana 3:8″……..kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi ″.
                Hiyo pia ndiyo kazi uliyopewa ndio maana anasema wewe u rungu langu na silaha zangu za vita.
Ø Fahamu udhaifu wako na umkabidhi Yesu udhaifu wako.
                -[2korintho.12:7-10] Mungu au Yesu wetu huwa anatafuta madhaifu yetu ili adhihirishe uwezo na ukuu wake kwetu.Wakati huo huo Shetani naye anatafuta udhaifu wako ili autumie kukumaliza nao.Hivyo ni lazima utambue udhaifu wako na uukabidhi kwa Mungu kabla shetani haujautumia kukuangamiza nao.
                         Fahamu kuwa hakuna kitu kibaya kama adui yako kujua madhaifu yako,ni hatari sana!.Unajua shetani aliufahamu udhaifu wa petro kuwa ni muongeaji sana[Mathayo.16:22-23].Alifahamu udhaifu wa Yuda kuwa ni mpenda pesa[Yohana.12:4-6].Aliufahamu udhaifu wa Daudi,wa Suleiman nk.Na hata wakwako anaufahamu;sasa cha kukusaidia ni kwamba mkabidhi Mungu madhaifu yako yote kuanzia leo.Pengine udhaifu wako ni ugonjwa fulani hakikisha unaukabidhi kwa Yesu kama Paulo alivyofanya[2korintho.12:7-10].Kumbuka kuwa kabla ya Paulo hajaufahamu udhaifu wake na kuukabidhi kwa Bwana,shetani aliutumia udhaifu huo kumtesa nao Paulo[soma vizuri 2korintho.12:7-10].Embu fikiria kuwa kila unapotaka kuanza maombi unaanza kusikia maumivu au kuumwa;sasa kama hufahamu huo ndio mwiba(udhaifu)wako ambao shetani anautumia kukutesa nao ili usiweze kupambana na yeye. 
Ø Fahamu kuwa dhambi ndiyo mlango wa shetani kuingilia sehemu          au Eneo fulani la maisha yako .Mwanzo.3:-
Ø Fahamu kuwa toba ya Damu ya Yesu ni muhimu sana kila siku kwa  ajili ya maombi yako juu ya mji/kanisa na familia yako hivyo jizoeze kuitumia kila siku.
Ø Kila mahali utapokanyaga kwa unyayo wa miguu yako, Bwana amekupa wewe kumiliki eneo hilo.Yoshua 1:3
                NB:Haya ni mambo ya msingi sana ya kuyazingatia kabla haujaingia kwenye vita ya rohoni dhidi ya shetani; kuna mengine mengi ya kujua  kupitia Roho mtakatifu na kusoma kwako neno la Mungu.
v Sasa baada ya kujitambua/fahamu wewe mwenyewe,pia tambua au fahamu  haya yafuatayo:-
                 i)Fahamu ni nani unayepambana naye(yaani adui yako)[efeso.6:12]
                   ii)Ni silaha gani anazotumia,adui yako
               iii)Mbinu gani anazitumia kukushinda(hila)[2korintho.2:11,Mwanzo.3].
                           Siri kubwa ya ushindi wa shetani kwetu ni dhambi;na pasipokuwa na dhambi si rahisi shetani kupata nafasi; kwa hiyo dhambi ni mlango mkubwa wa shetani kuingia sehemu yeyote.Ukiona mji unamilikiwa na adui ujue kuwa kuna dhambi ilifanyika ikamfungulia shetani mlango wa   kutawala.Mfano mzuri ni wa Ayubu; shetani alitafuta mlango wa kumvamia ayubu lakini Ayubu alikuwa akifanya maombi ya toba kila siku kwa ajili ya watoto wake na kwa ajili yake yeye mwenyewe.[Ayubu.1:5-10a].Toba ya Ayubu ilimtengenezea wigo/ukuta wa moto ambao shetani alishindwa kuuvuka.[Zekaria.2:5].
           
                            SEHEMU YA TATU.
                Aina za falme 2 katika ulimwengu wa roho (kutoka   sehem ya 2).
                 1:UFALME WA MUNGU(NURU)
                 2:UFALME WA SHETANI(GIZA).
                 Kama nilivyotangulia kusema katika sahemu ya pili kwamba zko falme mbili katika ulimwengu wa roho.Na ili falme hizi zote mbili ziweze kuwa na full control (umiliki)wa Eneo husika ni lazima wafanikiwe kumiliki Anga,Ardhi na watu.
                         Note vitu hivi:-
             a)–ufalme usio na watu sio ufalme,
             b)–ufalme usio na mipaka yake sio ufalme,
             c)–ufalme usiokuwa na umiliki wa anga sio  ufalme.
                               Kwa hiyo ili falme moja kati ya hizi  ziweze kuthibitika ni lazima zimiliki Anga,Ardhi na watu eneo husika.Hii inamaanisha kuwa ili shetani aweze kuwa na full control ya Eneo husika ni lazima amiliki anga ,Ardhi na watu.Anapofanikiwa kufanya hivyo; ufalme wake unathibitika,na yeye ndio anakuwa mfalme wa eneo hilo.
                            Sehemu ya anga ndiko shetani anapowaweka wakuu wake wa utawala wake yaani wakuu wa giza-mf.belizebuli.(Biblia ya kiingereza inasema "Evil spirits who overrules the kingdom…..)roho zitawalazo.marko.3:27,mat.12:29.Yesu anawatambulisha kama “mtu mwenye nguvu”.Ukitaka kufahamu ni jinsi gani hao wakuu walivyo fananisha na jinsi lilivyo jeshi letu(ranking);huwa kuna amiri jeshi mkuu(rais),mkuu wa majeshi,majenerali,luten,kapten nk.Kwa sababu mimi si mwanajeshi,nadhani ni vyema ukimpata mwanajeshi yeyote yeye anaweza kukuelezea zaidi mtiririko mzuri wa hierarchy ya jeshi.
                           Hii inamaanisha kuwa katika kila mji nchi,familia,kanisa nk.shetani ameweka wakuu wake(mf.jinsi rais wa nchi anavyoweka wakuu wa mkoa katika kila mkoa)-kumbuka kuwa nimekuambia kuwa wakuu hao (wa anga) ni ile  roho au zile roho zinazotawala eneo husika,sanasana ile iliyoanza kuwepo kwenye eneo hilo.
                           -Kwa hiyo ufalme wowote kati ya hizi mbili unapofanikiwa kuteka eneo lolote basi jua kuwa Anga,Ardhi na Watu wote watamilkiwa na ufalme huo.
                          Daniel.10:12-13,20. Kufanikiwa kwa Daniel na wale wenzake ni kutokana na maombi yao juu ya mji na nchi waliyokuwa wanaishi(Babeli).Daniel alipata kibali mbele ya mfalme wa babeli,lakini viongozi wengine wa taifa lile hawakufurahia na ndio maana walitunga hila ya kumuua ili wao wapate nafasi ile[Daniel.6].
                           Esta.3- Hamani alitaka kuwau wayahudi wote kwasababu tu alichukia kumwona mordekai na esta katika uongozi, kilichowaokoa wayahudi ni maombi yao.Wayahudi walichukiwa kwasababu sheria zao zilikuwa zinapingana na sheria za miungu ya akina hamani.
             Katika nyakati za leo,kama tutashindwa kuombea miji,nchi na maeneo tunayoishi, itakuwa ni vigumu sana kupata viongozi wazuri.Kwasababu asilimia kubwa ya maeneo tunayoishi yako chini ya utawala wa giza.Na utawala wa giza wakiwemo wachawi hawako tayari kuona miji au maeneo yao yanamilikiwa na viongozi kutoka kambi ya Adui(ukristo(waliookoka).Maana wanajua kuwa kiongozi akiwa ni wa kutoka kambi ya upinzani(ukristo) basi utawala wao uta pata shida.       NB:Tatizo kubwa walilonalo wanamaombi wengi katika kuomba kwa ajili ya Mungu kutupa viongozi wazuri , ni kwamba wanasubiria mpaka vyama vya siasa vimewachagulia viongozi, ndio wao  wanaanza kumwomba Mungu awape kiongozi mzuri kati ya wale waliochaguliwa na chama.Kumbuka kuwa chama hakina Mungu na wazee wengi wa vyama hawana Mungu na ndio wao wanaopanga mwaka ujao raisi awe nani hata kama ni mbaya wanachojali wao ni masilahi yao na ya chama nasio ya nchi.Kama tunataka kiongozi mzuri katika nchi yetu ya Tanzania au katika miji tunayoishi, ni lazima tuanze kuwaombea kuanzia leo kabla ya mwaka 2015. 

                    Utatambuaje jina la mkuu wa giza(anga-mtu mwenye nguvu)                 anayemiliki eneo unaloishi?
·        Angalia ni matendo gani ya giza yametawala eneo hilo.
                    Kwa mfano:utakuta katika mji Fulani uchawi ndio umeenea sana na hata habari zinazozungumziwa ni uchawi na uganga;wakati mwingine utakuta mji unasifika kwa vitendo vya mauaji,uzinzi/uasherati,ajali mafarakano na ulevi na vifo vya kiroho.Kwa namna nyingine unaweza ukatambua jina la mkuu wa giza(anga) wa eneo unaloishi kwa kuangalia ule uovu ulioanza kabla ya maovu mengine ,kumbuka kuwa kila uovu unaotendeka kuna pepo nyuma yake;uzinzi unasababishwa na pepo la uzinzi.                                                                                                                                                                                                                                                                   -Mara nyngi unapokuta sehemu kuna mafarakano ujue umesababishwa na mapepo kama ya kiburi,majivuno,uchawi na uhasi.
v [Daniel.10:12-13;20].
                           Kitabu hiki cha danieli kinatuonyesha kuwa aliyekuwa anamiliki anga la uajemi na uyunani ni ufalme wa giza.Na ndio maana wakina Daniel na wenzake walikuwa wakipigwa vita kwa sababu walikuwa wanaenda kinyume na ufalme uliokuwa unatawala anga la uajemi-babeli(yaani ufalme wa giza).Na ndio maana wakina meshack,shedrack na abedinego walitupwa kwenye tanuru la moto na Daniel akatupwa kwenye tundu la simba.
                          Na kwa kwaida siku zote shetani anawatumia wanadamu wenzetu katika kukamilisha kazi zake hapa duniani-mf.kule Babeli-aliwatumia viongozi.Na ndio maana mtume Paulo anatuambia kuwa tuombee wale wanaotutawala(viongozi).
                         Kwa hiyo ili ufanikiwe na kazi ya Mungu ifanikiwe ni lazima ujifunze kuombea mji unaoishi;kinyume na hapo ni kutokufanikiwa na kupigwa vita kila siku.Kwa hiyo usipomiliki anga na ardhi,kwa kweli utakosa Breakthrough(mpenyo) katika maombi yako na hata kwenye mafaniko kimaisha,kimasomo,kibiashara na kwenye huduma yako[kiroho na kimwili].Pia fahamu kuwa mfalme humiliki kwa maneno yake –yeye huwa anaagiza tu kwamba ifanyike alafu inafanyika.Pia wafalme kipindi cha agano la kale walikwenda vitani;kwa hiyo nawewe unatakiwa uingie vitani inapobidi.[1Nyak.20:1, 2Nyak.20:20-23]
                     Nb: Kufanikiwa kwa Mji unaoishi ndipo na wewe utakapofanikiwa kwa hiyo usiache kuuombea,na kuutakia amani mji huo unaoishi.
                       Yeremia.29:5-7 inasema hivi “Jengeni nyumba mkakae humo….kautakieni amani mji ule….mkauombee Kwa Bwana, Kwa maana katika amani ya mji huo ninyi mtapata amani”   
                             Wewe kama mfalme wa eneo unaloishi ni lazima uhakikishe kunakuwa na usalama juu ya watu wako(raia) aliokupa Bwana ,pia uhakikishe kuna ulinzi wa kutosha kwenye anga,ardhini na majini(toba ya damu ya Yesu kila siku juu ya maeneo hayo).Kumbuka kuwa mwanzo nilikuambia kuwa huduma hii ya ufalme haiendi au haijitegemei peke yake bali inategemea huduma ya ukuhani yenye upatanisho ndani yake na katika kuhakikisha ulinzi wa maeneo hayo manne yaani ardhi,anga,watu na maji na maeneo unayoishi, ni lazima huduma ya ukuhani iingie kazini.
                                      KAZI YA UKUHANI :
·        Kufanya maombi ya toba kwa ajili ya ardhi,anga,maji(bahari,mito na maziwa) pamoja na watu,kuta na malango ili kutakasa.[Neh.12:30]
·        Kufanya maombi ya upatanisho-ili kurejesha mahusiano ya mwanzo yaliyopotea baina ya Mungu na watu wake na eneo husika.[kut.32:32]
·        Kutengeneza mahali palipobomoka na kuzuia hasira ya Bwana kwa njia ya Toba ya Damu ya Yesu.[Eze.22:30-31]
                           -Kusimama mahali palipomoka maana yake ni kusimama katikati ya.Maana yake unasimama katikati ya Mungu na ndugu zako au mtu mwingine ambaye unataka kumwombea toba au maombi yoyote na pia kusimama katikati ya Mungu na mji au nchi yako,mfano mzuri ni ibrahim[Mwanzo.18,19].Kwa hiyo Mungu amekuinua wewe kama mwombezi kwa ajili ya mji,kanisa,familia na nchi uliyoko na hata biashara za eneo hilo.
·        Wewe kama kuhani unapoombea mji au nchi(ardhi,anga,na watu) ni lazima ujue jinsi ya kuwaombea watu hao na mji huo,yaani omba kama mama au mzazi anayemwombea mtoto wake(omba kama unajiombea mwenyewe).Na mfano mzuri ni maombi ya Musa naya Daniel[Daniel.9:4-19]. Maana Mungu anamtafuta mtu wa kufanya maombi ya kikuhani kama ya Daniel.[Eze.22:30-31],au ya Musa[Kut. 32:32].
                       Pia fahamu kuwa unapookoka unakuwa mfalme na kuhani maana yake ndugu zako wote wako chini yako na pia mji na watu walioko ndani yake wote wapo chini yako.Wewe ndio mwenye final say & final decision(maamuzi ya mwisho).Maana yake ukisema “No” inakuwa “No” ukisema “Yes” inakuwa “Yes” ndio maana Mungu akakupa funguo za ufalme wa mbinguni [Mathayo 16:18-19].
                       Wewe kama kuhani,unayo nafasi mbele za bwana ya kumwomba Mungu kwamba Mungu awaokoe ndugu zako,yaani wasife katika dhambi na Mungu akafanya hivyo.Mfano,Ibrahim alimwomba Mungu amwokoe ndugu yake Lutu asipatwe na ile adhabu yamoto juu ya sodoma na gomora.[Mwanzo.18,19].Pia Musa aliomba Mungu asiwaangamize waisrael na Mungu akamsikia.pia Mungu anakuheshimu sana unapokuwa kuhani na mlinzi. [Eze.3:17-21].
                      Watu wengi wamekuwa wakifa kwa magonjwa,na wengine kwa ajali na huwa wengi wanakufa wakiwa na dhambi na direct wanakwenda motoni.Hii ni kwasababu makuhani na walinzi(wanamaombi) wameshindwa kusimama katika nafasi zao.

                        UTAJUAJE KUWA ANGA LINAMILKIWA NA ADUI?
              I: Upinzani mkubwa katika kumtumikia Mungu.
                           Utakuta kila unapojaribu kumtumikia Mungu;ndugu,jamii,bosi  kazini, wote wanakupiga vita.Marko.5:1;-katika sura hii unaweza ukadhani kuwa ni wale watu ndio walioamua kumfukuza  Yesu katika mji wao,la hasha hapana.Bali ni kwamba mji ule na anga lake na watu wake walikuwa wanatawaliwa na kumilikiwa na adui na ndio maana badala ya kufurahia muujiza ule na kumkaribisha Yesu kwa ajili ya muujiza alioufanya kwa yule mtu aliyekuwa ameshindikana kwa muda mrefu wao wakaamua kumfukuza kwenye kijiji chao.
             Matendo.4:1-5,18.
             II: Ugumu wa kuomba (mpenyo wa maombi unakuwa mdogo)
                      Mara nyingi utajikuta unashindwa kuomba; unapofika muda wa maombi unaanza kupatwa na usingizi mzito na muda mwingine unakuwa unapiga miayo tu.
              III:Vifo vingi vya kiroho na vya kimwili.
                    Watu wengi wanaokoka lakini baada ya muda mchache wote wanarudi nyuma.
              IV: Kupoa kiroho kwa watumishi na wanamaombi wengi.
                 -Utakuta watu walikuwa na kasi na juhudi katika wokovu lakini baada ya muda wanakuwa vuguvugu.ufunuo.3:14-21
               V: Kuenea kwa mafarakano kwenye kanisa, familia,miji,nchi n.k
                    -Makanisa mengi leo hii yamejawa na migogoro; wachungaji dhidi ya wazee wa kanisa wanagombana n.k
               VI: kushamiri kwa matendo ya giza(maovu)
                   -Kama anga linamilikiwa na adui si ajabu kukuta uzinzi, uasherati, ujambazi, uchawi na kila tendo chafu na ovu la giza.Yote hiyo ni kwasababu tayari mji huo umekuwa makazi ya mapepo.
                              Ufunuo.18:2 “…umeanguka,umeanguka Babeli ule mkuu;umekuwa maskani ya mashetani,na ngome ya kila roho mchafu,na kila ndege mchafu mwenye kuchukiza”
                      -Hizi ni baadhi ya alama chache tu za kujua kama Anga linatawaliwa na Adui au la!      

                    KWA NINI UMILIKI MJI(ARDHI,WATU NA ANGA LAKE?
                    I: Lazima umiliki mji,anga n.k, kwa sababu wewe ni mfalme tena ni kuhani wa Bwana.Na kama wewe ni mfalme na kuhani wa Bwana kama biblia isemavyo katika kitabu cha;Ufunuo.5:9-10,Basi ujue  kuna eneo ambalo wewe unatakiwa ulitawale kama mfalme wa eneo hilo.
                       Na ili ufalme wako uweze kuwa na nguvu ni lazima umiliki Anga,Ardhi,na Watu.Kinyume na hapo ufalme wako hauwezi kuthibitika na ufalme huo uko mashakani-wewe unafikiri ni kwasababu gani Tanzania tuna jeshi la Anga,nchi kavu,majini n.k- Jibu ni kwasababu ya kulinda Anga,ardhi,maji na raia wa Tanzania-na ndio maana  ni lazima ujizoeze kuombea Anga,Ardhi,maji na watu wa sehemu unakoishi.
                       Usipoombea mji na Anga unakoishi basi jua kuwa utakuwa kila siku unapigwa vita na kukutana na vikwazo kwenye kumtumikia kwako Mungu, kwenye uchumi, afya yako,na biashara yako n.k.Yesu alisema kesheni muombe msije mkaingia majaribuni[Mathayo.26:41].
                     Hivyo kama unataka breakthrough (mpenyo) kwenye maisha yako ya kiroho na ya kimwili ni lazima umiliki mji,watu na anga la eneo unaloishi;ukishindwa kufanya hivyo basi jua utapata vita kubwa sana,kiroho na kimwili.
             II:Kwasababu kufanikiwa kwa mji unaoishi ndipo na wewe utakapofanikiwa kiroho na kimwili.Yeremia.29:5-7.
                    -unapoombea mji unaoishi utasababisha kuuepushia mji huo na maangamizi na majanga kama vile ajali,vita,mafuriko,moto,tsunami n.k
·        Ezekiel.22:30, Bwana anamtafuta mtu atakaye simama ili kuuombea mji ili hasira ya bwana isimwagwe kwenye mji.ukisoma vizuri sura hii ya ezekiel.22 utaona kuwa kinachosababisha Bwana atake kumwaga hasira yake ni kwa sababu ya maovu kama uzinzi, rushwa n.k
·        Isaya.62:6-7,Bwana anasema kuwa ameweka walinzi juu ya mji wa yerusalemu.Pia katika mji unaoishi Bwana ameweka walinzi na mmoja wapo akiwa ni wewe.Na unapokubali kuwa mlinzi ni lazima uwe unaomba maombi haya “ufalme wako na uje na mapenzi yako yatimizwe…”.Ufalme wake uje wapi?ni kwenye mji unaoishi.
                     -Hii inamaanisha kuwa unapoomba maombi haya ufalme wa Mungu unakuja na kumiliki na kutawala mji, anga lake, na watu waishio ndani yake.
                      Lakini kabla ufalme wa Mungu haujaja ni lazima utumie hiyo nafasi ya ukuhani uliyopewa kwa ajili ya kutengeneza na kutaarisha mazingira ya ujio wa ufalme wa Mungu kwenye mji unaoishi.Yaani uachilie maombi ya toba ya Damu ya Yesu kwenye mji,ardhi yake,anga lake na watu wake.
                   -Nehemia .12:30, inasema hivi; “Na makuhani na walawi wakajitakasa, wakawatakasa watu, malango na kuta”
             Toba yako ya mara kwa mara + Maombi ya kuombea ufalme wa Mungu uje kwenye eneo unaloishi.Yatakufanya umiliki mji na anga la eneo unaloishi.
              III: Kwasababu sisi ni uzao wa ibrahimu.
                 -Bwana alimwambia ibrahimu kuwa wazao wako watamilki malango ya Adui zao na miji ya adui zao.Mwanzo.22:

                                         SEHEMU YA NNE(4):KANUNI…
                JINSI YA KUTEKA NA KUANZA KUMILIKI MJI NA ANGA AMBALO ADUI AMESHALISHIKILIA TAYARI.
·        Kwanza fahamu jambo hili kuwa aliyeumba Dunia, mbingu (anga) na vyote vijazavyo ni Mungu.Hii inamaanisha kwamba hata mji unaokaa ni Mungu ndiye aliyeuumba, hata sehemu anakoishi shetani ni Mungu (YESU) ndiye aliyeumba vyote hivyo.Yoh.1:1-5. “…..vyote vilifanyika kwa huyo,wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika….”
                       -Kwa hiyo shetani hakuumba chochote bali yeye aliumbwa tu.Zaidi sana  alichokiumba yeye ni dhambi na maovu tu.Hivyo unapoona anamiliki eneo fulani jua kuwa; kuna uhalali au kibali fulani amekipata kutokana na dhambi na maovu yaliyotendwa na yanayotendwa na watu katika mji husika(huo).
                     -Shetani ni mvamizi ni sawasawa na jinsi wakoloni walivyofanya kwa waafrika, kwa kuwavamia na kuwatawala.Kwahiyo unapoona shetani analimiliki eneo fulani jua kuwa ana haki/uhalali fulani ameupata kutokana na maovu na madhambi yanayotendeka katika mji huo.Pengine ni mazindiko yaliyofanywa na mababu,uzinzi,uchawi unaotendeka kila siku n.k.
·        Mathayo.4:8.  
                     -Wewe unafikiri ujasiri huo shetani aliutoa wapi wa kuthubutu kumwambia muumbaji  wake(Yesu)[Yohana 1:1-5]kuwa akimsujudia yeye atampa mali zote za ulimwengu huu.
                    -Shetani alipata uhalali wa kumiliki Dunia hii baada ya dhambi ya akina Adamu na hawa.
                   -Ili sasa uweze kulimilikiAnga sharti au kwanza ufanye toba ya Damu ya Yesu kwa ajili ya Eneo hilo.unapo achilia maombi ya toba ya Damu ya Yesu, kwenye Eneo lako kinachotokea ni kwamba ule uhalali wa shetani wa kumiliki hilo Eneo unaondolewa au unafutwa na damu ya Yesu .Halleluya!.
                     Baada ya kufanya maombi ya Toba ili kuliteka Eneo hilo ni lazima ujue jinsi ya kufunga wakuu wa giza(Anga) na kuwaseta kuzimu
                                            Marko.3:27, Mathayo 12:29.
                     Kabla sijaendelea labda nikukumbushe kuwa hawa wakuu wa giza mara nyingi hukaa kwenye maeneo matatu hapa duniani.
             i).Kwenye Anga-roho hizi chafu zinazotawala Eneo kubwa mfano; nchi, miji n.k hukaa kwenye Anga.
                Mfano:Daniel 10:12-13,20.
                 -Mkuu wa ufalme wa uajemi
           ii).Roho chafu zitawalazo ndani ya kanisa familia n.k
                  -Hawa hukaa ndani ya mtu kutokana na uhalali  walioupata kutoka kwa wazazi,mababu,na dhambi alizozitenda mtu huyo au hukaa katika anga pia.
           iii).Ardhini.
                      -uhalali wa kukaa kwenye ardhi wanaupata kutokana na  
                 matambiko,mazindiko na makafara yanayotolewa kila siku.
                Mfano: marko.5 yule mtu aliyemilikiwa na jeshi la mapepo.
     
               UFANYE NINI ILI UFANIKISHE UTEKAJI WA MJI HUO.
                     Sasa basi ili uweze kuteka mji,anga n.k na kuumiliki ni lazima kwanza uwe umeshafanya toba ya Damu ya Yesu, kwa ajili -yako,ndugu zako na kuachilia ulinzi wa Damu ya Yesu} mji,anga,ardhi na kwa ajili ya watu wa mji huo.Hatua ya pili ni kuvaa silaha[Efeso.6:13-18]Baada ya hayo sasa umfunge mtu mwenye nguvu-mkuu wa giza(Anga) wa eneo hilo-[Mathayo. 12:29] kwa kutumia funguo (mamlaka) uliyopewa na Yesu;ya kufunga na kufungua[Mathayo. 16:19].
                         -Na ndio maana Yesu alitufundisha mbinu za kufanya ili tuweze kuteka eneo lolote,kupitia kitabu cha marko.3:27,mathayo 12:29. “Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu,na kuviteka vitu vyake,asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu;ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
              -Pia Yesu alitupa nguvu ya kufunga na kufungua jambo lolote la adui.
                         Mathayo 16:18-19 “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme mbinguni;na lolote utakalolifunga duniani,litakuwa limefungwa mbinguni;na lolote utakalolifungua duniani,litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
                     Pia anasema milango ya kuzimu haitalishinda kanisa langu.
                      -Na tayari Bwana alishasema kuwa atatupa sisi tulio wa uzao wa Ibrahimu kumiliki malango ya Adui zetu.
                       Mwanzo 22:17. “…….na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”
v Mungu ametuokoa ili tuanze kueneza ufalme wake; na ili kueneza ufalme wa Mungu ni lazima tuteke miji na maeneo mbali mbali ili yaweze kuwa chini ya ufalme wa Mungu.Kwa hiyo kila eneo unalokwenda ni lazima uliteke na kulimiliki kwa ajili ya ufalme wa MUNGU.
v Tumezaliwa tuwe washindi na watekaji wa mji(conquerors)[Rumi.8:37,Mwanzo 24:60,1Yoh. 5:4]
v Kila mahali unapokanyaga, Bwana amekupa wewe kumiliki.Joshua 1:3
v Pia Yesu ametupa sisi mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule Adui na hakuna kitakachotuzuru
                        Luka .10:19; Rumi. 16:20
                      -Miji tunayoishi ni lazima ifikie hatua iitwe kwa jina la Bwana .Eze.45:35- na sio kwa jina la mapepo kama ilivyokuwa kwa Babeli[Ufunuo.18:2] “…umeanguka,umeanguka Babeli ule mkuu;umekuwa maskani ya mashetani,na ngome ya kila roho mchafu,na kila ndege mchafu mwenye kuchukiza”
                      -Mji unapokosa maombi unakuwa ni ngome ya mapepo kama ilivyo kuwa kwa babel.
             NB:Mji unapokosa maombi unakuwa kama jalala la kila aina uchafu wa dhambi.Unajua,mapepo ninayafananisha na nzi au panya-kwa kawaida huwezi ukakuta nzi,panya mahali palipo pasafi mara nyingi utawakuta sehemu chafuchafu kama jalalani.Wanachofuata inzi ni uchafu na ndivyo walivyo mapepo na majini.Mahali ambapo maombi ya toba ya Damu ya Yesu yanafanyika kila siku,sio rahisi ukute utawala wa shetani.

KANUNI YA MAOMBI HAYA NI:-
·        Mathayo 12:29 + Mathayo 16:18-19=mathayo.6:9b-10
KUFUNGA (BINDING).
                   Tunapozungumzia suala la kufunga, hapa maana yake ni kama vile unavyomkamata mwizi alafu ukamfunga miguu na mikono –ndivyo unavyotakiwa kuwafunga hawa watu wenye nguvu (roho zitawalazo) mathayo. 12:29.
                       Tunajua kuwa Yesu alikuja ili kuzivunja kazi za adui-ibilisi. 1Yohana 3:8
Kufungua (loosing).
                Shetani huwa anatabia ya kufunga watu kwa roho za mauti,magonjwa, uzinzi n.k.Kwa hiyo umepewa fursa hizo ili uwafungue watu waliofungwa-isaya.61:1-4.
                     -Neno la Mungu ni silaha,upanga wa roho.
·        Luka 13:11-12, 15-16
·        Efeso.6:17b, ebra.4:12
·        -Fahamu jambo hili kwenye vita hii unachokiri/kisema kwa kinywa chako kinakwenda kuwa cha kwako-ukikiri kushindwa lazima utashindwa tu.ufunuo.12:11
             ″ nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao″
             Kwa hiyo =NENO + DAMUYA YESU=USHINDI.
             Mathayo 4:1-11.
                   Yesu alimshinda shetani kwa kutumia upanga wa roho (Neno la     Mungu).Kwa hiyo hakikisha kuwa umejaa neno ndani yako na ulitumie neno kwenye maombi yako ya kufunga hao watu wenye nguvu. mathayo. 12:29.

             HUU NI MFANO MZURI WA MAOMBI YA KUMFUNGA MTU    MWENYE NGUVU(mfano.Belizebul-kumfunga belzebuli)
                    -Kumbuka kabla ya maombi haya hakikisha umeshafanya toba kama ya Daniel.9 alafu sasa ujivike silaha za Mungu-Efeso.6:13-18. tamka kwa kinywa chako mwenyewe kuwa “ninajifunga mshipi wa kweli kiunoni mwangu kwa jina la Yesu,navaa drii ya haki kifuani mwangu,najifungia utayari miguuni mwangu kwa ajili ya injili ya amani,zaidi ya yote ninatwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo nitaizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu,napokea chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu,nami nadumu katika sala zote na maombi nikisali kila wakati katika Roho…”
                        -Baada ya hapo anza kufunga mkuu wa Anga na baada ya hapo fanya unachotaka kama ni kubomoa-bomoa, kuharibu-haribu na kisha,angamiza  n.k.lakini usisahau kujenga na kupanda kitu,kila unapobomoa na kuharibu na kuangamiza.
             Mfano.umevunja roho ya mauti –hakikisha unatamka(unapanda)roho ya uzima.[Yer.1:10,12,Yoh.10:10b]

                Huu ni mfano wa maombi haya;
                  Omba hivi:-               
                                  Ninafunga roho ya uchawi iliyokaa katika Anga kwa minyororo na kwa pingu za chuma zitokazo mbinguni .Ninasimama katika neno la Mungu la Math.16:18-19.ambao unasema “ nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa Mbinguni na kila utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni- (Math.16:19) nami ninakufunga mikono na miguu kwa jina la Yesu na kwa hilo neno la BWANA.Nami ninakata kila kiunganishi chochote kinachounganisha mkuu wa mapepo( rulling spirit-mkuu wao)na mapepo madogomadogo .Nami ninakung’oa  wewe mkuu wa giza katika anga hili ninakushusha na kukukanyaga katika jina la Yesu.Ninalitakasa Anga hili kwa Damu ya Yesu, nami namkabidhi Roho mtakatifu achukue nafasi ya kuwa mkuu wa Anga la Eneo(taja jina la eneo unaloliombea)                                                          
                           - Nami ninavunja roho za zote za ajali, mauti, uchawi, mafarakano, uzinzi, matambiko na makafara kwa damu ya Yesu ninateketeza  na kuziharibu kwa jina la Yesu kristo.maana mimi ni rungu la bwana sawasawa naYeremia 51:20-23 Bwana ameniweka ili kuvunja vunja kazi zako,kama neno lake linavosema katika -1Yohana 3:8 “kwamba kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili apate kuzivunja kazi zote za ibilisi shetani “nami kwa Damu Yesu ninavunja kazi zako zote juu ya maisha yangu,mji huu,biashara yangu,afya yangu n.k.
                           -Nami katika jina la Yesu ninajifunika na kujificha ndani ya damu ya YESU,Ee Mungu ninaomba unizungushie ukuta wa moto sawaswa na neno lako la zekaria.2:5.Ninampinga shetani na roho zake zote za malipizi na visasi alizozikusuda juu yangu na juu ya ndugu zangu,biashara yangu,masomo yangu,afya yangu na chochote kilicho chini yangu;shetani ninakutangazia kuwa huna mamlaka juu yake kwa jina na kwa Damu ya YESU.Ninasimamia neno la bwana la Isaya.54:14-17 linalosema(soma)katika jina la Yesu nimeomba na kushukuru ameni”

             Nb:Huu ni msingi tu wa kukusaidia kuanzia; ila haufungwi kutumia kanuni nyingine  ambazo Roho mtakatifu atakufundisha kupitia kusoma kwako neno.

                               MUHIMU:Baada ya Maombi hayo:-
·        Omba ulinzi wa Mungu juu yako na juu ya ndugu zako.
·        Vunja roho zote za malipizi na visasi vinavyokusudiwa na Adui juu ya maisha yako na ndugu zako
·        Soma neno hili- Isaya 54:14-17(ulinzi dhidi ya roho za malipizi na visasi)[Zekaria 2:5]
           -Mshukuru Mungu kwa kuwa ameshajibu maombi yako katika jina la Yesu.
                      SHORT SUMMARY.
               MFUMO WA MAOMBI YAKO(MTIRIRIKO) UNATAKIWA UWE HIVI:-
      A.Toba ya Damu ya YesuIsa.1:18,43:25
·        Tubu kwa ajili ya ndugu zako,wewe mwenyewe marafiki na watu   wote wa karibu yako,omba ulinzi kwa ajili yako na ndugu zako.
·        Tubu kwa ajili ya Mji wako,Anga lake ,Ardhi n.k.   takasa na umwage Damu ya Yesu ya ulinzi ya kufunika Anga,Mji,Ardhi,Barabara,maji n.k
              B.KUOMBEA MJI,KANISA FAMILIA N.K
             -Tumia funguo za Mathayo 16:19,18:18 funga wakuu wa giza ,Anga na mapepo wabaya kwenye Anga n.k
             Wasete kuzimu kwa jina na kwa Damu ya YESU.
             -kata kila connection(kiunganishi) inayowaunganisha wakuu wa giza na mapepo wadogowadogo.
                     -vunja kazi za ibilisi [1Yohana3:8,Yeremia 51:20-23]
                       C.HITIMISHO.
             Ulinzi juu yako, ndugu zako ,vunja roho ya malipizi na visasi-Isa.54:14 17. “……watu watakaokusanyana juu yako wataanguka……….kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa…..”
             Nb:Kama bado maneno hayo yote ya biblia hayajakaa kichwani,basi hakikisha unakuwa na biblia karibu; kila unapofanya maombi yako ya aina hii.

                                  Neno la Mwisho.
                     Maombi yako ni ya muhimu sana kwa ajili ya huduma hii kuendelea kusonga mbele.philip.3:13-14. “Ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika ila natenda neno moja tu;…nikiyachuchumilia yaliyo mbele;nakaza mwendo nifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika kristo Yesu”
             Kwa maoni na ushauri na maswali ;
            JESUS ACTS MINISTRIES &JESUS BLOOD’S                       INTERCESSORY MINISTRIES.[JAM &JBIM]
                    Mwl.loyshiye.k.mollel
                 Mob.+255762568280
              Email.kisotaloyshiye@gmail.com